Proverbs 21
1Moyo wa mfalme uko katika mkono wa Bwana; 2 huuongoza kama mkondo wa maji, popote apendapo. 1
2Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake, 2 bali Bwana huupima moyo. 1
3Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika 2 zaidi kwa Bwana kuliko dhabihu. 1
4Macho ya kudharau na moyo wa kiburi, 2 ambavyo ni taa ya waovu, vyote ni dhambi! 1
5Mipango ya mwenye bidii huelekeza kwenye faida, 2 kama vile kwa hakika pupa huelekeza kwenye umaskini. 1
6Mali iliyopatikana kwa ulimi wa uongo 2 ni mvuke upitao upesi na mtego wa kufisha. 1
7Jeuri ya waovu itawaburuta mbali, 2 kwa kuwa wanakataa kufanya yaliyo sawa. 1
8Njia ya mwenye hatia ni ya upotovu, 2 bali tabia ya mtu asiye na hatia ni nyofu. 1
9Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba, 2 kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi. 1
10Mtu mwovu hutamani sana ubaya, 2 jirani yake hapati huruma kutoka kwake. 1
11Wakati mwenye mzaha ameadhibiwa, 2 mjinga hupata hekima; 1 wakati mtu mwenye hekima afundishwapo, 2 hupata maarifa. 1
12Mwenye Haki huyajua yanayotendeka katika nyumba za waovu, 2 naye atawaangamiza waovu. 1
13Mtu akiziba masikio asisikie kilio cha maskini, 2 yeye pia atalia, wala hatajibiwa. 1
14Zawadi itolewayo kwa siri hutuliza hasira 2 na rushwa iliyofichwa kwenye nguo hutuliza ghadhabu kali. 1
15Wakati haki imetendeka, huleta furaha kwa wenye haki, 2 bali kitisho kwa watenda mabaya. 1
16Mtu anayepotea kutoka mapito ya ufahamu, 2 hupumzika katika kundi la waliokufa. 1
17Mtu apendaye anasa atakuwa maskini, 2 yeyote apendaye mvinyo na mafuta kamwe hatakuwa tajiri. 1
18Waovu huwa fidia kwa ajili ya wenye haki, 2 nao wasio waaminifu kwa ajili ya wanyofu. 1
19Ni afadhali kuishi jangwani 2 kuliko kuishi na mke mgomvi na mkorofi. 1
20Katika nyumba ya mwenye hekima 2 kuna akiba ya vyakula vizuri na mafuta, 1 lakini mtu mpumbavu 2 hutafuna vyote alivyo navyo. 1
21Yeye afuatiaye haki na upendo 2 hupata uzima, mafanikio na heshima. 1
22Mtu mwenye hekima huushambulia mji wa wenye nguvu, 2 na kuangusha ngome wanazozitegemea. 1
23Yeye alindaye kinywa chake na ulimi wake 2 hujilinda na maafa. 1
24Mtu mwenye kiburi na majivuno, “Mdhihaki” ndilo jina lake; 2 hutenda mambo kwa kiburi kilichozidi. 1
25Kutamani sana kwa mvivu kutakuwa kifo chake, 2 kwa sababu mikono yake haitaki kufanya kazi. 1
26Mchana kutwa hutamani zaidi, 2 lakini mnyofu hutoa pasipo kuzuia. 1
27Dhabihu ya mtu mwovu ni chukizo, 2 si zaidi sana itolewapo kwa nia mbaya! 1
28Shahidi wa uongo ataangamia, 2 bali maneno ya mwenye kusikia yatadumu. 1
29Mtu mwovu ana uso wa ushupavu, 2 bali mtu mnyofu huzifikiria njia zake. 1
30Hakuna hekima, wala akili, wala mpango 2 unaoweza kufaulu dhidi ya Bwana. 1
31Farasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita, 2 bali ushindi huwa kwa Bwana.