Proverbs · Biblia (Kiswahili)

Proverbs 29

1Mtu anayeendelea kuwa na shingo ngumu baada ya maonyo mengi, 2 ataangamia ghafula, wala hapati dawa. 1

2Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi; 2 waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni. 1

3Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake, 2 bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake. 1

4Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti, 2 bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza. 1

5Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili, 2 anautandaza wavu kuitega miguu yake. 1

6Mtu mbaya hutegwa na dhambi yake mwenyewe 2 bali mwenye haki huweza kuimba na kufurahi. 1

7Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini, 2 bali mwovu hajishughulishi na hilo. 1

8Wenye mzaha huuchochea mji, 2 bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira. 1

9Kama mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu, 2 mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani. 1

10Watu wamwagao damu humchukia mtu mwadilifu 2 na hutafuta kumuua mtu mnyofu. 1

11Mpumbavu huonyesha hasira yake yote, 2 bali mwenye hekima hujizuia. 1

12Kama mtawala akisikiliza uongo, 2 maafisa wake wote huwa waovu. 1

13Mtu maskini na mtu anayeonea wanafanana kwa jambo hili: 2 Bwana hutia nuru macho yao wote wawili. 1

14Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki, 2 kiti chake cha enzi kitakuwa thabiti siku zote. 1

15Fimbo ya maonyo hutia hekima, 2 bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo 2 humwaibisha mama yake. 1

16Wakati waovu wanapostawi, 2 pia dhambi vivyo hivyo, 2 lakini wenye haki wataliona anguko lao. 1

17Mrudi mwanao, naye atakupa amani, 2 atakufurahisha nafsi yako. 1

18Mahali pasipo na ufunuo, watu kujizuia, 2 bali ana heri mtu yule aishikaye sheria. 1

19Mtumishi hawezi kuonywa kwa maneno matupu, 2 ajapoelewa, hataitikia. 1

20Je, unamwona mtu azungumzaye kwa haraka? 2 Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko yeye. 1

21Kama mtu akimdekeza mtumishi wake tangu ujanani, 2 atamletea sikitiko mwishoni. 1

22Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi, 2 naye mtu mwenye hasira ya haraka 2 hutenda dhambi nyingi. 1

23Kiburi cha mtu humshusha, 2 bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu 2 hupata heshima. 1

24Anayekubaliana na mwizi ni adui wa nafsi yake mwenyewe; 2 huapishwa lakini hathubutu kushuhudia. 1

25Kuwaogopa watu huwa ni mtego, 2 bali yeyote amtumainiaye Bwana atakuwa salama. 1

26Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala, 2 bali mtu hupata haki kutoka kwa Bwana. 1

27Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu; 2 waovu huwachukia sana wenye haki.

← Proverbs 28Read In The App, Free →Proverbs 30 →

Study Proverbs 29

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031