Proverbs 17
1Afadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu 2 kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi. 1
2Mtumishi mwenye hekima atatawala juu ya mwana aaibishaye, 2 naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu. 1
3Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu, 2 bali Bwana huujaribu moyo. 1
4Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya; 2 mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara. 1
5Yeye anaye mdhihaki maskini huonyesha dharau kwa Muumba wake; 2 yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa. 1
6Wana wa wana ni taji la wazee, 2 nao wazazi ni fahari ya watoto wao. 1
7Midomo yenye uwezo wa ushawishi haimfai mpumbavu: 2 je, ni mibaya kiasi gani zaidi midomo ya uongo kwa mtawala! 1
8Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; 2 kokote kigeukiapo, hufanikiwa. 1
9Yeye anayesamehe kosa hudumisha upendo, 2 bali yeyote arudiaye jambo hutenganisha marafiki wa karibu. 1
10Karipio humwingia sana mtu mwenye kutambua 2 kuliko mapigo mia kwa mpumbavu. 1
11Mtu mbaya hupenda kuasi tu; 2 mjumbe asiye na huruma atatumwa dhidi yake. 1
12Ni afadhali ukutane na dubu aliyenyangʼanywa watoto wake, 2 kuliko mpumbavu katika upumbavu wake. 1
13Ikiwa mtu atalipa baya kwa jema, 2 kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba yake. 1
14Kuanzisha ugomvi ni kama kutoboa bwawa la maji; 2 kwa hiyo acha jambo hilo kabla mabishano hayajaanza. 1
15Yeye asemaye kuwa asiye na haki ana haki, 2 naye asemaye kuwa mwenye haki hana haki: 2 Bwana huwachukia sana wote wawili. 1
16Fedha ina faida gani mikononi mwa mpumbavu, 2 wakati yeye hana haja ya kupata hekima? 1
17Rafiki hupenda wakati wote 2 naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida. 1
18Mtu mjinga hupana mkono ili kuweka rehani, 2 naye huweka dhamana kwa jirani yake. 1
19Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi; 2 naye ainuaye sana lango lake + 17:19 Kuinua lango maana yake ni kusema kwa majivuno. hutafuta uharibifu. 1
20Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa; 2 naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu huanguka kwenye taabu. 1
21Kuwa na mwana mpumbavu huleta huzuni; 2 hakuna furaha kwa baba wa mpumbavu. 1
22Moyo wenye furaha ni dawa nzuri, 2 bali roho iliyopondeka hukausha mifupa. 1
23Mtu mwovu hukubali rushwa kwa siri 2 ili kupotosha njia ya haki. 1
24Mtu wa ufahamu huitazama hekima, 2 lakini macho ya mpumbavu huhangaika 2 hadi kwenye miisho ya dunia. 1
25Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake 2 na uchungu kwa yeye aliyemzaa. 1
26Si vizuri kumwadhibu mtu asiye na hatia, 2 au kuwapiga sana maafisa kwa ajili ya uadilifu wao. 1
27Mtu mwenye maarifa hutumia maneno kwa kujizuia, 2 naye mtu mwenye ufahamu ana moyo wa utulivu. 1
28Hata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima kama akinyamaza, 2 na mwenye ufahamu kama akiuzuia ulimi wake.