Proverbs 1
1Mithali za Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli: 1
2Kwa kupata hekima na nidhamu; 2 kwa kufahamu maneno ya busara; 1
3kwa kujipatia nidhamu na busara, 2 kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea; 1
4huwapa busara wajinga, 2 maarifa na akili kwa vijana; 1
5wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao, 2 wenye kupambanua na wapate mwongozo; 1
6kwa kufahamu mithali na mifano, 2 misemo na vitendawili vya wenye hekima. 1
7Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa, 2 lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. 1 Onyo Dhidi Ya Ushawishi Wa Marafiki Waovu 1
8Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako, 2 wala usiyaache mafundisho ya mama yako. 1
9Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako, 2 na mkufu wa kuipamba shingo yako. 1
10Mwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi, 2 usikubaliane nao. 1
11Kama wakisema, “Twende tufuatane; 2 tukamvizie mtu na kumwaga damu, 2 njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia; 1
12tuwameze wakiwa hai kama kaburi, + 1:12 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. 2 wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni. 1
13Tutapata aina zote za vitu vya thamani 2 na kujaza nyumba zetu kwa nyara. 1
14Njoo ushirikiane nasi, 2 vitu vyote tutakavyopata tutagawana.” 1
15Mwanangu, usiandamane nao. 2 Usiweke mguu wako katika njia zao, 1
16kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi, 2 ni wepesi kumwaga damu. 1
17Tazama ni jinsi gani ilivyo kazi bure kutandaza wavu 2 wakati ndege wote wanakuona! 1
18Watu hawa huvizia kumwaga damu yao wenyewe; 2 hujivizia tu wenyewe! 1
19Huu ndio mwisho wa wote ambao wanajipatia mali kwa hila; 2 huuondoa uhai wa wale wenye mali. 1 Onyo Dhidi Ya Kukataa Hekima 1
20Hekima huita kwa sauti kuu barabarani, 2 hupaza sauti yake kwenye viwanja vikubwa; 1
21kwenye makutano ya barabara za mji 2 zenye makelele mengi hupaza sauti, 2 kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake: 1
22“Enyi wajinga, mtangʼangʼania ujinga wenu hadi lini? 2 Mpaka lini wenye mizaha watafurahia mizaha, 2 na wapumbavu kuchukia maarifa? 1
23Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu, 2 ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu 2 na kuwafahamisha maneno yangu. 1
24Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita 2 na hakuna yeyote aliyekubali 2 niliponyoosha mkono wangu, 1
25kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote 2 na hamkukubali karipio langu, 1
26mimi nami nitawacheka katika maafa yenu, 2 nitawadhihaki wakati janga litawapata: 1
27wakati janga litawapata kama tufani, 2 wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli, 2 wakati dhiki na taabu zitawalemea. 1
28“Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu; 2 watanitafuta lakini hawatanipata. 1
29Kwa kuwa walichukia maarifa, 2 wala hawakuchagua kumcha Bwana, 1
30kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu, 2 na kukataa maonyo yangu, 1
31watakula matunda ya njia zao, 2 na watashibishwa matunda ya hila zao. 1
32Kwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua, 2 nako kuridhika kwa wajinga kutawaangamiza. 1
33Lakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama, 2 atatulia, bila kuwa na hofu ya madhara.”