Job · Biblia (Kiswahili)

Job 10

1“Nayachukia sana haya maisha yangu; 2 kwa hiyo nitatoa malalamiko yangu kwa wazi bila kujizuia, 2 nami nitanena kutokana na uchungu wa moyo wangu. 1

2Nitamwambia Mungu: Usinihukumu, 2 bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu. 1

3Je, inakupendeza wewe kunionea, 2 kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako, 2 huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu? 1

4Je, wewe una macho ya kimwili? 2 Je, wewe huona kama mwanadamu aonavyo? 1

5Je, siku zako ni kama zile za mwanadamu, 2 au miaka yako ni kama ile ya mtu, 1

6ili kwamba utafute makosa yangu 2 na kuichunguza dhambi yangu; 1

7ingawa wajua kuwa mimi sina hatia, 2 na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako? 1

8“Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunifanya. 2 Je, sasa utageuka na kuniangamiza? 1

9Kumbuka kuwa ulinifinyanga kama udongo wa mfinyanzi. 2 Je, sasa utanifanya kuwa mavumbi tena? 1

10Je, wewe hukunimimina mimi kama maziwa, 2 na kunigandisha kama jibini, 1

11ukanivika ngozi na nyama, 2 na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa? 1

12Umenipa uhai na kunitendea wema, 2 katika uangalizi wako umeilinda roho yangu. 1

13“Lakini hili ndilo ulilolificha moyoni mwako, 2 nami ninajua kuwa hili lilikuwa katika nia yako: 1

14Kama nilifanya dhambi, ungekuwa umeniona, 2 wala usingeacha kosa langu lipite bila kuadhibiwa. 1

15Kama nina hatia, ole wangu! 2 Hata kama ningekuwa sina hatia, 2 siwezi kukiinua kichwa changu, 1 kwa kuwa nimejawa na aibu, 2 na kuzama katika mateso yangu. 1

16Kama nikiinua kichwa changu juu, unaninyatia kama simba, 2 na kuonyesha tena uwezo wa kutisha dhidi yangu. 1

17Wewe waleta mashahidi wapya dhidi yangu 2 na kuzidisha hasira yako juu yangu; 2 nazo nguvu zako zinanijia wimbi moja baada ya jingine. 1

18“Kwa nini basi ulinitoa tumboni? 2 Ninatamani ningekufa kabla jicho lolote halijaniona. 1

19Laiti nisingekuwako kamwe, 2 au ningekuwa nimechukuliwa moja kwa moja 2 kutoka tumboni kwenda kaburini! 1

20Je, siku zangu chache si zimekaribia kuisha? 2 Niachie ili niweze kupata muda mfupi wa kufurahi 1

21kabla sijaenda mahali ambapo hakuna kurudi tena, 2 katika nchi ya giza na uvuli wa mauti, 1

22nchi ya giza kuu sana, 2 yenye uvuli wa giza na machafuko, 2 mahali ambapo hata nuru ni giza.”

← Job 9Read In The App, Free →Job 11 →

Study Job 10

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142