Job · Biblia (Kiswahili)

Job 12

1Ndipo Ayubu akajibu: 1

2“Bila shaka ninyi ndio watu, 2 nayo hekima itakoma mtakapokufa! 1

3Lakini mimi ninao ufahamu kama ninyi; 2 mimi si duni kwenu. 2 Ni nani asiyejua mambo haya yote? 1

4“Nimekuwa mtu wa kuchekwa na rafiki zangu, 2 ingawa nilimwita Mungu naye akanijibu: 1 mimi ni mtu wa kuchekwa tu, 2 ingawa ni mwadilifu na nisiye na hatia! 1

5Wanadamu wakiwa katika utulivu huwa na dharau kwa wale wenye msiba 1 kana kwamba ndiyo haki ya wale ambao miguu yao inateleza. 1

6Hema za wanyangʼanyi hazisumbuliwi, 2 wale wanaomghadhibisha Mungu wako salama: 2 wale wamchukuao mungu wao mikononi mwao. 1

7“Lakini ulizeni wanyama, nao watawafundisha, 2 au ndege wa angani, nao watawaambia; 1

8au zungumzeni na dunia, nayo itawafundisha, 2 au acheni samaki wa baharini wawape taarifa. 1

9Ni nani miongoni mwa hawa wote asiyejua 2 kwamba mkono wa Bwana ndio uliofanya hili? 1

10Mkononi mwake kuna uhai wa kila kiumbe, 2 na pumzi ya wanadamu wote. 1

11Je, sikio haliyajaribu maneno 2 kama vile ulimi uonjavyo chakula? 1

12Je, hekima haipatikani katikati ya wazee? 2 Je, maisha marefu hayaleti ufahamu? 1

13“Hekima na nguvu ni vya Mungu; 2 shauri na ufahamu ni vyake yeye. 1

14Kile anachokibomoa hakiwezi kujengeka tena; 2 mtu aliyefungiwa naye hawezi kufunguliwa. 1

15Akizuia maji, huwa pana ukame; 2 akiyaachia maji, huharibu nchi. 1

16Kwake kuna nguvu na ushindi; 2 adanganywaye na adanganyaye, wote wawili ni wake. 1

17Yeye huwaondoa washauri wakiwa wametekwa nyara, 2 naye huwapumbaza wanaotoa maamuzi. 1

18Huondoa pingu zilizofungwa na wafalme, 2 na kuwafunga mishipi ya kiunoni. 1

19Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara, 2 na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu. 1

20Hunyamazisha midomo ya washauri wanaoaminika, 2 na kuondoa busara ya wazee. 1

21Huwamwagia dharau wanaoheshimika, 2 na kuwavua silaha wenye nguvu. 1

22Hufunua mambo ya ndani ya gizani, 2 na kuyaleta nuruni yale yaliyositirika sana. 1

23Huyafanya mataifa yatukuke na kuyaangamiza; 2 hufanya mataifa kuwa makubwa, naye huyatawanya. 1

24Huwaondolea viongozi wa nchi akili zao; 2 huwapeleka watangetange nyikani pasipo na njia. 1

25Hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga; 2 huwafanya wapepesuke kama walevi.

← Job 11Read In The App, Free →Job 13 →

Study Job 12

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142