Job 24
1“Kwa nini Mwenyezi asiweke nyakati kwa ajili ya hukumu? 2 Kwa nini wale wamjuao wazitafute siku kama hizo bila mafanikio? 1
2Watu husogeza mawe ya mpaka; 2 huchunga makundi ya wanyama waliyonyangʼanya kwa nguvu. 1
3Huwanyangʼanya yatima punda wao, 2 na kumchukua rehani fahali wa mjane. 1
4Humsukuma mhitaji kutoka njia, 2 na kuwafanya maskini wote wa nchi kulazimika kujificha. 1
5Kama punda-mwitu jangwani, 2 maskini huzunguka katika kazi zao za kutafuta chakula; 1 mahali palipo jangwa 2 huwapa chakula cha watoto wao. 1
6Hukusanya chakula mashambani na kuokota masazo 2 katika mashamba ya mizabibu ya waovu. 1
7Kwa kukosa nguo, usiku kucha hukaa uchi; 2 hawana chochote cha kujifunika baridi. 1
8Hutota kwa mvua za mlimani, 2 nao huikumbatia miamba kwa ajili ya kukosa pa kujisitiri. 1
9Mtoto yatima hupokonywa matitini; 2 mtoto wachanga wa maskini hunyakuliwa kwa ajili ya deni. 1
10Kwa kukosa nguo, hutembea uchi; 2 hubeba miganda ya ngano, lakini huwa na njaa. 1
11Hukamua zeituni katika mawe ya kusagia; 2 hukanyaga mashinikizo, lakini wanaona kiu. 1
12Kilio cha huzuni cha wanaokufa kinapaa kutoka mjini, 2 nazo nafsi za waliojeruhiwa zinalilia msaada. 1 Lakini Mungu hamlaumu mtu yeyote 2 kwa kutenda mabaya. 1
13“Wako wale wanaoiasi nuru, 2 wasiofahamu njia zake 2 wala hawakai katika mapito yake. 1
14Wakati mwanga wa mchana unapotoweka, muuaji huinuka 2 naye huwaua maskini na mhitaji; 2 wakati wa usiku hunyemelea kama mwizi. 1
15Jicho la mzinzi hungojea wakati wa giza, 2 naye hufikiri, ‘Hakuna jicho litakaloniona,’ 2 naye huuficha uso wake. 1
16Katika giza, huvunja majumba, 2 lakini wakati wa mchana hujifungia ndani; 2 hawataki kufanya lolote nuruni. 1
17Kwa wote hawa, giza nene ndiyo asubuhi yao; 2 hujifanya rafiki na vitisho vya gizani. 1
18“Lakini wao ni povu juu ya maji; 2 sehemu yao juu ya nchi imelaaniwa, 1 hivyo hakuna hata mmoja 2 aendaye kwenye shamba la mizabibu. 1
19Kama vile joto na hari vinyakuavyo theluji iliyoyeyuka, 2 ndivyo kuzimu kuwanyakuavyo waliotenda dhambi. 1
20Tumbo lililowazaa huwasahau, 2 nao huwa karamu ya mabuu; 1 watu waovu hawakumbukwi tena, 2 lakini huvunjika kama mti. 1
21Huwafanya mawindo wanawake tasa na wasio na watoto, 2 nao hawaonyeshi huruma kwa wajane. 1
22Lakini Mungu huwakokota wenye nguvu kwa uwezo wake; 2 ingawa wamestawi, hawana hakika ya maisha. 1
23Aweza akawaacha wakapumzika wakijihisi salama, 2 lakini macho yake yanaona njia zao. 1
24Kwa kitambo kidogo hutukuka, hatimaye hutoweka; 2 hushushwa na kukusanywa kama wengine wote, 2 hukatwa kama masuke ya nafaka. 1
25“Kama hili sivyo, ni nani awezaye kunithibitisha kuwa mwongo, 2 na kuyafanya maneno yangu kuwa si kitu?”