Job 37
1“Kwa hili moyo wangu unatetemeka, 2 nao unaruka kutoka mahali pake. 1
2Sikiliza! Sikiliza ngurumo ya sauti yake, 2 sauti ya ngurumo itokayo kinywani mwake. 1
3Huuachilia umeme wake wa radi chini ya mbingu yote 2 na kuupeleka hata miisho ya dunia. 1
4Baada ya hayo huja sauti ya ngurumo yake; 2 Mungu hunguruma kwa sauti yake ya fahari. 1 Wakati sauti yake ingurumapo tena, 2 huuachilia umeme wake wa radi. 1
5Sauti ya Mungu hunguruma kwa namna za ajabu; 2 yeye hutenda mambo makuu kupita ufahamu wetu. 1
6Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya dunia,’ 2 nayo manyunyu ya mvua, ‘Uwe mvua ya nguvu.’ 1
7Ili wanadamu wote aliowaumba wapate kujua kazi zake, 2 yeye humzuilia kila mtu shughuli zake. 1
8Wanyama hujificha; 2 hubakia kwenye mapango yao. 1
9Dhoruba hutoka katika chumba chake, 2 baridi hutoka katika upepo uendao kasi. 1
10Pumzi ya Mungu hutoa barafu, 2 eneo kubwa la maji huganda. 1
11Huyasheheneza mawingu kwa maji, 2 naye husambaza umeme wake wa radi kupitia hayo. 1
12Nayo mawingu huzungukazunguka pande zote kwa amri yake, 2 juu ya uso wa dunia yote, 2 kufanya lolote ayaamuruyo. 1
13Huleta mawingu ili kuadhibu wanadamu, 2 au kuinyeshea dunia yake na kuonyesha upendo wake. 1
14“Ayubu, sikiliza hili; 2 nyamaza na uyafikiri maajabu ya Mungu. 1
15Je, unajua jinsi Mungu anavyoyaongoza mawingu, 2 na kufanya umeme wake wa radi utoe mwanga? 1
16Je, wajua jinsi mawingu yanavyokaa yakiwa yametulia, 2 hayo maajabu yake yeye aliye mkamilifu katika maarifa? 1
17Wewe unayeshindwa na joto katika nguo zako 2 wakati nchi imenyamazishwa kimya bila upepo wa kusini, 1
18je, waweza kuungana naye katika kuzitandaza anga, 2 zilizo ngumu kama kioo cha shaba ya kuyeyushwa? 1
19“Tuambieni yatupasayo kumwambia; 2 hatuwezi kutayarisha shauri letu kwa sababu ya ujinga wetu. 1
20Je, aambiwe kwamba nataka kuongea? 2 Je, yuko mtu ambaye angeomba kumezwa? 1
21Basi hakuna awezaye kulitazama jua, 2 jinsi linavyongʼaa angani, 2 upepo ukishafagia mawingu. 1
22Kutoka kaskazini yeye huja na fahari kuu; 2 Mungu huja katika utukufu wa kutisha. 1
23Yeye Mwenyezi hatuwezi kumfikia, naye ametukuzwa katika uweza; 2 katika hukumu zake na haki yake kuu, hataonea. 1
24Kwa hiyo, wanadamu mheshimuni, 2 kwa kuwa yeye hamstahi yeyote anayejidhania kuwa ana hekima.”