Job · Biblia (Kiswahili)

Job 14

1“Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke 2 siku zake ni chache nazo zimejaa taabu. 1

2Huchanua kama ua kisha hunyauka; 2 huwa kama kivuli kipitacho upesi, wala hadumu. 1

3Je, unamwekea jicho lako mtu kama huyo? 2 Je, utamleta mbele yako katika hukumu? 1

4Ni nani awezaye kutoa kitu safi kutoka kitu najisi? 2 Hakuna awezaye! 1

5Siku za mwanadamu zimewekewa mpaka; 2 umekwisha kutangaza idadi ya miezi yake 2 na kuweka mpaka ambao hawezi kuuvuka. 1

6Hivyo angalia mbali umwache, 2 hadi awe amekamilisha muda wake 2 kama mtu aliyeajiriwa. 1

7“Kwa maana lipo tumaini kwa mti; 2 kama ukikatwa utachipuka tena, 2 nayo machipukizi yake mapya hayatakoma. 1

8Mizizi yake yaweza kuchakaa ardhini 2 na kisiki chake kufa udongoni, 1

9lakini kwa kupata dalili ya maji utachipua 2 na kutoa machipukizi kama mche. 1

10Lakini mwanadamu hufa, na huo ndio mwisho wake; 2 hutoa pumzi ya mwisho, naye hayuko tena! 1

11Kama vile maji yatowekavyo katika bahari, 2 au mkondo wa mto ukaushwavyo na kuwa mkavu, 1

12ndivyo mwanadamu alalavyo chini asiamke; 2 hadi mbingu zitakapokuwa hazipo tena, 1 wanadamu hawataamka au kuamshwa 2 kutoka kwenye usingizi wao. 1

13“Laiti kama ungenificha kaburini, + 14:13 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. 2 na kunisitiri hadi hasira yako ipite! 1 Laiti ungeniwekea wakati, 2 na kisha ukanikumbuka! 1

14Je, kama mtu akifa, aweza kuishi tena? 2 Siku zote za kazi zangu ngumu 2 nitangojea kufanywa upya kwangu. 1

15Utaniita nami nitakuitika; 2 utakionea shauku kiumbe ambacho mikono yako ilikiumba. 1

16Hakika ndipo utakapozihesabu hatua zangu, 2 lakini hutazifuatia dhambi zangu. 1

17Makosa yangu yatafungiwa kwa lakiri kwenye mfuko, 2 nawe utazifunika dhambi zangu. 1

18“Lakini kama mlima umomonyokavyo na kufikichika 2 na kama vile mwamba uondolewavyo mahali pake, 1

19kama maji yamalizavyo mawe, 2 na mafuriko yachukuavyo udongo, 2 ndivyo unavyoharibu tegemeo la mwanadamu. 1

20Humshinda mara moja kwa daima, naye hutoweka; 2 waibadilisha sura yake na kumwondoa. 1

21Kama wanawe wakipewa heshima, yeye hafahamu; 2 kama wakidharauliwa, yeye haoni. 1

22Yeye hasikii kingine isipokuwa maumivu ya mwili wake mwenyewe, 2 naye huomboleza kwa ajili yake mwenyewe.”

← Job 13Read In The App, Free →Job 15 →

Study Job 14

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142