Job 15
1Kisha Elifazi Mtemani akajibu: 1
2“Je, mtu mwenye hekima hujibu kwa mawazo matupu, 2 au kujaza tumbo lake kwa upepo wenye joto wa mashariki? 1
3Je, aweza kubishana juu ya maneno yasiyofaa, 2 kwa hotuba zisizo na maana? 1
4Lakini unadhoofisha hata uchaji wa Mungu 2 na kuzuia ibada mbele za Mungu. 1
5Dhambi yako inasukuma kinywa chako, 2 nawe umechagua ulimi wa hila. 1
6Kinywa chako mwenyewe kinakuhukumu, wala si changu; 2 midomo yako mwenyewe inashuhudia dhidi yako. 1
7“Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa? 2 Ulizaliwa kabla ya vilima? 1
8Je, wewe husikiliza mashauri ya siri ya Mungu? 2 Je, wewe unaizuia hekima iwe yako mwenyewe? 1
9Wewe unajua kitu gani tusichokijua sisi? 2 Unafahamu kitu gani tusichokifahamu sisi? 1
10Wale wenye mvi na wazee wako upande wetu, 2 watu ambao ni wazee hata kuliko baba yako. 1
11Je, faraja za Mungu hazikutoshi, 2 au maneno yaliyosemwa kwako kwa upole si kitu? 1
12Kwa nini moyo wako unakudanganya, 2 na kwa nini macho yako yanangʼaa, 1
13ili kwamba upate kutoa hasira yako dhidi ya Mungu, 2 na kumwaga maneno kama hayo kutoka kinywani mwako? 1
14“Mwanadamu ni kitu gani, hata aweze kuwa safi, 2 au yeye aliyezaliwa na mwanamke, hata aweze kuwa mwadilifu? 1
15Kama Mungu hawaamini watakatifu wake, 2 kama hata mbingu zenyewe si safi machoni pake, 1
16sembuse mwanadamu ambaye ni mwovu na mpotovu, 2 ambaye hunywa uovu kama anywavyo maji! 1
17“Nisikilize mimi nami nitakueleza, 2 acha nikuambie yale niliyoyaona, 1
18ambayo watu wenye hekima wameyanena, 2 bila kuficha lolote walilopokea toka kwa baba zao 1
19(wakati ambao wao peke yao ndio walipewa nchi, 2 hakuna mgeni aliyepita miongoni mwao): 1
20Mtu mwovu siku zake zote hupata mateso, 2 miaka yote aliwekewa mkorofi. 1
21Sauti za kutisha hujaa masikioni mwake; 2 katika kufanikiwa kwake, wanyangʼanyi humshambulia. 1
22Hukata tamaa kuokoka gizani; 2 amewekwa kwa ajili ya upanga. 1
23Hutangatanga, akitafuta chakula; 2 anajua kwamba siku ya giza iko karibu. 1
24Taabu na maumivu makuu vinamtia hofu; 2 humshinda kama mfalme aliye tayari kwa vita, 1
25kwa sababu amemkunjia Mungu ngumi yake 2 na kujigamba dhidi ya Mwenyezi, 1
26kwa kiburi akishambulia dhidi ya Mungu 2 akiwa na ngao nene, iliyo imara. 1
27“Ingawa uso wake umefunikwa na mafuta kwa unene 2 na kiuno chake kimevimba kwa kunenepa, 1
28ataishi katika miji ya magofu, 2 na katika nyumba ambazo haziishi mwanadamu yeyote, 2 nyumba zinazokuwa vifusi. 1
29Hatatajirika tena, nao utajiri wake hautadumu, 2 wala mali zake hazitakuwa nyingi juu ya nchi. 1
30Hatatoka gizani; 2 mwali wa moto utanyausha machipukizi yake, 2 nayo pumzi ya kinywa cha Mungu itamwondolea mbali. 1
31Asijidanganye mwenyewe kutumainia ubatili, 2 kwa kuwa hatapata malipo yoyote. 1
32Atakuwa amelipwa kikamilifu kabla ya wakati wake, 2 nayo matawi yake hayatastawi. 1
33Atafanana na mzabibu uliopukutishwa matunda yake kabla hayajaiva, 2 kama mzeituni unaodondosha maua yake. 1
34Kwa kuwa jamii ya wasiomcha Mungu watakuwa tasa, 2 nao moto utateketeza hema za wale wanaopenda rushwa. 1
35Hutunga mimba ya madhara na kuzaa uovu; 2 matumbo yao huumba udanganyifu.”