Job · Biblia (Kiswahili)

Job 18

1Bildadi Mshuhi akajibu: 1

2“Je, ni lini utafika mwisho wa maneno haya? 2 Uwe mwenye busara, nasi ndipo tutakapoweza kuongea. 1

3Kwa nini sisi tunafikiriwa kama wanyama, 2 na kuonekana wajinga machoni pako? 1

4Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande 2 katika hasira yako, 1 je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe? 2 Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake? 1

5“Taa ya mwovu imezimwa, 2 nao mwali wa moto wake umezimika. 1

6Mwanga hemani mwake umekuwa giza; 2 taa iliyo karibu naye imezimika. 1

7Nguvu za hatua zake zimedhoofishwa; 2 shauri lake baya litamwangusha. 1

8Miguu yake imemsukumia kwenye wavu, 2 naye anatangatanga kwenye matundu ya wavu. 1

9Tanzi litamkamata kwenye kisigino; 2 mtego utamshikilia kwa nguvu. 1

10Kitanzi kimefichwa ardhini kwa ajili yake; 2 mtego uko kwenye njia yake. 1

11Vitisho vimemtia hofu kila upande, 2 na adui zake humwandama kila hatua. 1

12Janga linamwonea shauku; 2 maafa yako tayari kwa ajili yake aangukapo. 1

13Nayo yatakula sehemu ya ngozi yake; 2 mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake. 1

14Atangʼolewa kutoka usalama wa hema lake, 2 na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho. 1

15Moto utakaa katika hema lake; 2 moto wa kiberiti utamwagwa juu ya makao yake. 1

16Mizizi yake chini itakauka 2 na matawi yake juu yatanyauka. 1

17Kumbukumbu lake litatoweka katika dunia, 2 wala hatakuwa na jina katika nchi. 1

18Ameondolewa nuruni na kusukumiwa gizani, 2 naye amefukuzwa mbali atoke duniani. 1

19Hana mtoto wala mzao miongoni mwa watu wake, 2 wala aliyenusurika mahali alipoishi. 1

20Watu wa magharibi watashangaa yaliyompata; 2 watu wa mashariki watapatwa na hofu. 1

21Hakika ndivyo yalivyo makao ya mtu mwovu; 2 ndivyo palivyo mahali pake mtu asiyemjua Mungu.”

← Job 17Read In The App, Free →Job 19 →

Study Job 18

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142