Job 36
1Elihu akaendelea kusema: 1
2“Nivumilie kidogo zaidi nami nitakuonyesha 2 kwamba yako mengi zaidi ya kusemwa kwa ajili ya Mungu. 1
3Ninayapata maarifa yangu kutoka mbali, 2 nami nitamhesabia haki Muumba wangu. 1
4Uwe na hakika kwamba maneno yangu si ya uongo; 2 mmoja aliye mkamilifu katika maarifa yuko pamoja na wewe. 1
5“Mungu ni mwenye nguvu, lakini hamdharau mwanadamu; 2 ni mwenye nguvu, naye ni thabiti katika shauri lake. 1
6Hawaachi waovu waendelee kuishi, 2 bali huwapa walioteswa haki yao. 1
7Yeye haondoi macho yake kwa wenye haki; 2 huwaketisha penye viti vya enzi pamoja na wafalme 2 na kuwatukuza milele. 1
8Lakini ikiwa watu wamefungwa kwenye minyororo, 2 wakiwa wameshikiliwa na kamba za mateso, 1
9huwaonyesha yale waliyoyatenda, 2 kwamba wametenda dhambi kwa majivuno. 1
10Huwafanya wao kusikia maonyo, 2 na huwaagiza kutubu uovu wao. 1
11Kama wakitii na kumtumikia, 2 wataishi siku zao zilizobaki katika mafanikio, 2 na miaka yao katika utoshelevu. 1
12Lakini wasiposikiliza, 2 wataangamia kwa upanga, 2 nao watakufa pasipo maarifa. 1
13“Wasiomcha Mungu moyoni mwao huficha chuki; 2 hata anapowafunga, hawamwombi msaada. 1
14Wanakufa wangali vijana, 2 miongoni mwa wanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu. 1
15Bali wao wanaoteseka huwaokoa katika mateso yao, 2 na kuzungumza nao katika dhiki zao. 1
16“Yeye anakubembeleza utoke katika mataya ya dhiki, 2 ili kukuweka mahali palipo na nafasi mbali na kizuizi, 2 hadi kwenye meza yako ya faraja iliyojaa vyakula vizuri. 1
17Lakini sasa umelemewa na hukumu kwa ajili ya uovu; 2 hukumu na haki vimekukamata. 1
18Uwe mwangalifu ili yeyote asikushawishi kwa utajiri; 2 usipotoshwe kwa fungu kubwa la rushwa. 1
19Je, utajiri wako hata nguvu zako nyingi 2 vinaweza kukusaidia usiingie kwenye dhiki? 1
20Usiutamani usiku uje, 2 ili uwaburute watu mbali na nyumba zao. 1
21Jihadhari usigeukie uovu, 2 ambao unaupenda zaidi kuliko mateso. 1
22“Mungu ametukuzwa katika nguvu zake. 2 Ni nani aliye mwalimu kama yeye? 1
23Ni nani aliyemwelekeza katika njia zake, 2 au kumwambia, ‘Wewe umetenda yasiyo sawa’? 1
24Kumbuka kuzitukuza kazi zake, 2 ambazo watu wamezisifu katika wimbo. 1
25Wanadamu wote wameiona; 2 watu wanaikazia macho kwa mbali. 1
26Tazama jinsi Mungu alivyo mkuu, 2 kupita ufahamu wetu! 2 Hesabu ya miaka yake haitafutiki. 1
27“Yeye huvuta juu matone ya maji, 2 ayachujayo kama mvua kutoka kwenye vijito; 1
28mawingu huangusha chini maji yake, 2 nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu. 1
29Ni nani ajuaye jinsi ayatandazavyo mawingu, 2 jinsi angurumavyo kutoka hemani mwake. 1
30Tazama jinsi anavyotandaza umeme wa radi kumzunguka, 2 naye huvifunika vilindi vya bahari. 1
31Hivi ndivyo atawalavyo mataifa, 2 na kuwapa chakula kwa wingi. 1
32Huujaza mkono wake kwa umeme wa radi, 2 na kuuagiza kulenga shabaha yake. 1
33Ngurumo zake hutangaza dhoruba inayokuja; 2 hata mifugo hujulisha kukaribia kwake. + 36:33 Au: hutangaza kuja kwake.