Job 9
1Kisha Ayubu akajibu: 1
2“Naam, najua hili ni kweli. 2 Lakini mwanadamu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? 1
3Ingawa mtu angetaka kushindana naye, 2 asingaliweza kumjibu Mungu hata mara moja miongoni mwa elfu moja. 1
4Hekima yake ni kubwa sana na ana uwezo mwingi mno. 2 Ni nani aliyempinga naye akawa salama? 1
5Aiondoa milima bila yenyewe kujua 2 na kuipindua kwa hasira yake. 1
6Aitikisa dunia kutoka mahali pake 2 na kuzifanya nguzo zake zitetemeke. 1
7Husema na jua, nalo likaacha kuangaza; 2 naye huizima mianga ya nyota. 1
8Yeye peke yake huzitandaza mbingu 2 na kuyakanyaga mawimbi ya bahari. 1
9Yeye ndiye Muumba wa nyota za Dubu, + 9:9 Nyota za Dubu hapa ina maana ya kundi la nyota za kaskazini, ambazo zinaitwa kwa jina la Dubu Mkuu. na Orioni, + 9:9 Orioni ni kundi la nyota kubwa. 2 Kilimia, + 9:9 Kilimia ni jina lililopewa nyota saba (Taurus). na makundi ya nyota za kusini. 1
10Hutenda maajabu yasiyopimika, 2 miujiza isiyoweza kuhesabiwa. 1
11Anapopita karibu nami, siwezi kumwona; 2 apitapo mbele yangu, simtambui. 1
12Anapochukua kwa ghafula, ni nani awezaye kumzuia? 2 Ni nani awezaye kumwambia, ‘Unafanya nini?’ 1
13Mungu hataizuia hasira yake; 2 hata jeshi kubwa la Rahabu + 9:13 Rahabu hapa ina maana ya Misri kwa fumbo. lenye nguvu 2 linajikunyata miguuni pake. 1
14“Ni vipi basi mimi nitaweza kubishana naye? 2 Nawezaje kupata maneno ya kuhojiana naye? 1
15Ingawa sikuwa na hatia, sikuweza kumjibu; 2 ningeweza tu kumsihi Mhukumu wangu anihurumie. 1
16Hata kama ningemwita kwenye shauri, naye akakubali, 2 siamini kama angenisikiliza. 1
17Yeye angeniangamiza kwa dhoruba 2 na kuongeza majeraha yangu pasipo na sababu. 1
18Asingeniacha nipumue 2 bali angenifunika kabisa na huzuni kuu. 1
19Kama ni suala la nguvu, yeye ni mwenye nguvu! 2 Kama ni suala la haki, ni nani awezaye kumwita mahakamani? 1
20Hata kama sikuwa na hatia, kinywa changu kingenihukumu; 2 kama sikuwa na kosa, kingenitangaza kuwa mwenye hatia. 1
21“Ingawa mimi sina kosa, 2 haileti tofauti katika nafsi yangu; 2 nauchukia uhai wangu. 1
22Hayo yote ni sawa; ndiyo sababu nasema, 2 ‘Yeye huwaangamiza wasio na makosa pamoja na waovu.’ 1
23Wakati pigo liletapo kifo cha ghafula, 2 yeye hudhihaki kule kukata tamaa kwa yule asiye na kosa. 1
24Wakati nchi inapoangukia mikononi mwa waovu, 2 yeye huwafunga macho mahakimu wake. 2 Kama si yeye, basi ni nani? 1
25“Siku zangu zapita mbio kuliko mkimbiaji; 2 zinapita upesi bila kuona furaha hata kidogo. 1
26Zinapita upesi kama mashua ya mafunjo, 2 mfano wa tai ayashukiaye mawindo kwa ghafula. 1
27Kama nikisema, ‘Nitayasahau malalamiko yangu, 2 nitabadili sura ya uso wangu na kutabasamu,’ 1
28bado ninahofia mateso yangu yote, 2 kwa kuwa ninajua hutanihesabu kuwa sina hatia. 1
29Kwa kuwa nimeonekana mwenye hatia, 2 kwa nini basi nitaabishwe bure? 1
30Hata kama ningejiosha kwa sabuni 2 na kutakasa mikono yangu kwa magadi, 1
31wewe ungenitupa kwenye shimo la utelezi 2 kiasi kwamba hata nguo zangu zingenichukia sana. 1
32“Yeye si mwanadamu kama mimi ili niweze kumjibu, 2 ili kwamba tuweze kushindana naye mahakamani. 1
33Laiti angelikuwepo mtu wa kutupatanisha kati yetu, 2 aweke mkono wake juu yetu sote wawili, 1
34mtu angeliiondoa fimbo ya Mungu juu yangu, 2 ili utisho wake usiendelee kunitia hofu. 1
35Ndipo ningenena naye, bila kumwogopa, 2 lakini kama ilivyo kwangu sasa, sitaweza.