Job 35
1Ndipo Elihu akasema: 1
2“Je, unadhani hili ni haki? 2 Wewe unasema, ‘Nina haki mbele za Mungu.’ 1
3Bado unamuuliza, ‘Ni faida gani nimepata, 2 na imenifaidi nini kwa kutokutenda dhambi?’ 1
4“Ningependa nikujibu wewe 2 pamoja na marafiki zako walio pamoja nawe. 1
5Tazama juu mbinguni ukaone; 2 yaangalie mawingu yaliyo juu sana juu yako. 1
6Je, ukitenda dhambi, inamdhuruje Mungu? 2 Kama dhambi zako zikiwa nyingi, 2 hilo linamfanyia nini Mungu? 1
7Kama wewe ni mwadilifu, unampa nini, 2 au yeye anapokea nini mkononi kwako? 1
8Uovu wako unamdhuru tu mtu mwingine kama wewe, 2 nayo haki yako inawafaa wanadamu tu. 1
9“Wanadamu hulia kwa kulemewa na mateso; 2 huomba msaada kutoka mkono wenye nguvu. 1
10Lakini hakuna asemaye, ‘Yuko wapi Mungu Muumba wangu, 2 yeye anifanyaye niimbe usiku, 1
11yeye atufundishaye sisi zaidi kuliko wanyama wa dunia, 2 na kutufanya wenye hekima kuliko ndege wa angani?’ 1
12Yeye hajibu wakati watu waliapo 2 kwa sababu ya kiburi cha watu waovu. 1
13Naam, Mungu hasikilizi maombi yao ya ubatili; 2 Mwenyezi hayazingatii. 1
14Si zaidi sana kwamba hatakusikiliza 2 wewe usemapo humwoni, 1 tena ya kwamba shauri lako liko mbele zake 2 na wewe lazima umngojee, 1
15pia zaidi, kwamba hasira yake kamwe haiadhibu 2 wala haangalii uovu hata kidogo? 1
16Hivyo Ayubu hufumbua kinywa chake kwa maneno yasiyo na maana; 2 anaongea maneno mengi bila maarifa.”