Job · Biblia (Kiswahili)

Job 8

1Kisha Bildadi Mshuhi akajibu: 1

2“Hata lini wewe utasema mambo kama haya? 2 Maneno yako ni kama upepo mkuu. 1

3Je, Mungu hupotosha hukumu? 2 Je, Mwenyezi hupotosha kile kilicho haki? 1

4Watoto wako walipomtenda dhambi, 2 aliwapa adhabu ya dhambi yao. 1

5Lakini ukimtafuta Mungu, 2 nawe ukamsihi Mwenyezi, 1

6ikiwa wewe ni safi na mnyofu, 2 hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako, 2 na kukurudisha katika mahali pako pa haki. 1

7Ijapokuwa mwanzo wako ulikuwa mdogo, 2 lakini mwisho wako utakuwa wa mafanikio. 1

8“Ukaulize vizazi vilivyotangulia 2 na uone baba zao walijifunza nini, 1

9kwa kuwa sisi tumezaliwa jana tu na hatujui lolote, 2 nazo siku zetu duniani ni kama kivuli tu. 1

10Je, hawatakufundisha na kukueleza? 2 Je, hawataleta maneno kutoka kwenye kufahamu kwao? 1

11Je, mafunjo yaweza kumea mahali pasipo na matope? 2 Matete yaweza kustawi bila maji? 1

12Wakati bado yanaendelea kukua kabla ya kukatwa, 2 hunyauka haraka kuliko majani mengine. 1

13Huu ndio mwisho wa watu wote wanaomsahau Mungu; 2 vivyo hivyo matumaini ya wasiomjali Mungu huangamia. 1

14Lile analolitumainia huvunjika upesi; 2 lile analolitegemea ni utando wa buibui. 1

15Huutegemea utando wake, lakini hausimami; 2 huungʼangʼania, lakini haudumu. 1

16Yeye ni kama mti ulionyeshewa vizuri wakati wa jua, 2 ukieneza machipukizi yake bustanini; 1

17huifunganisha mizizi yake kwenye lundo la mawe, 2 na kutafuta nafasi katikati ya mawe. 1

18Unapongʼolewa kutoka mahali pake, 2 ndipo mahali pale huukana na kusema, 2 ‘Mimi kamwe sikukuona.’ 1

19Hakika uhai wake hunyauka, 2 na kutoka udongoni mimea mingine huota. 1

20“Hakika Mungu hamkatai mtu asiye na hatia, 2 wala kuitia nguvu mikono ya mtenda mabaya. 1

21Bado atakijaza kinywa chako na kicheko, 2 na midomo yako na kelele za shangwe. 1

22Adui zako watavikwa aibu, 2 nazo hema za waovu hazitakuwepo tena.”

← Job 7Read In The App, Free →Job 9 →

Study Job 8

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142