Job 7
1“Je, mwanadamu hana kazi ngumu duniani? 2 Siku zake si kama zile za mtu aliyeajiriwa? 1
2Kama mtumwa anavyovionea shauku vivuli vya jioni, 2 au mtu aliyeajiriwa anavyoungojea mshahara wake, 1
3ndivyo nilivyogawiwa miezi ya ubatili, 2 nami nimeandikiwa huzuni usiku hata usiku. 1
4Wakati nilalapo ninawaza, ‘Itachukua muda gani kabla sijaamka?’ 2 Usiku huwa mrefu, nami najigeuzageuza hadi mapambazuko. 1
5Mwili wangu umevikwa mabuu na uchafu, 2 ngozi yangu imetumbuka na kutunga usaha. 1 Ayubu Anamlilia Mungu 1
6“Siku zangu zinapita upesi kuliko mtande wa kufuma, 2 nazo zinafikia mwisho wake bila matumaini. 1
7Kumbuka, Ee Mungu, maisha yangu ni kama pumzi; 2 macho yangu kamwe hayataona tena raha. 1
8Lile jicho linaloniona sasa halitaniona tena; 2 utanitafuta, wala sitakuwepo. 1
9Kama vile wingu liondokavyo na kutoweka, 2 vivyo hivyo yeye ashukaye kaburini + 7:9 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. harudi tena. 1
10Kamwe harudi tena nyumbani mwake; 2 wala mahali pake hapatamjua tena. 1
11“Kwa hiyo sitanyamaza; 2 nitanena kutokana na maumivu makuu ya roho yangu, 2 nitalalama kwa uchungu wa nafsi yangu. 1
12Je, mimi ni bahari, au mnyama mkubwa mno akaaye vilindini, 2 hata uniweke chini ya ulinzi? 1
13Ninapofikiri kwamba kitanda changu kitanifariji, 2 nacho kiti changu cha fahari kitapunguza malalamiko yangu, 1
14ndipo wanitisha kwa ndoto 2 na kunitia hofu kwa maono, 1
15hivyo ninachagua kujinyonga na kufa, 2 kuliko huu mwili wangu. 1
16Ninayachukia maisha yangu; nisingetamani kuendelea kuishi. 2 Niache; siku zangu ni ubatili. 1
17“Mwanadamu ni kitu gani hata umjali kiasi hiki, 2 kwamba unamtia sana maanani, 1
18kwamba unamwangalia kila asubuhi 2 na kumjaribu kila wakati? 1
19Je, hutaacha kamwe kunitazama, 2 au kuniacha japo kwa kitambo kidogo tu? 1
20Ikiwa nimetenda dhambi, nimekufanyia nini, 2 Ewe mlinzi wa wanadamu? 1 Kwa nini umeniweka niwe shabaha yako? 2 Je, nimekuwa mzigo kwako? 1
21Kwa nini husamehi makosa yangu 2 na kuachilia dhambi zangu? 1 Kwa kuwa hivi karibuni nitalala mavumbini; 2 nawe utanitafuta, wala sitakuwepo.”