Job 6
1Kisha Ayubu akajibu: 1
2“Laiti uchungu wangu ungeweza kupimwa, 2 nayo taabu yangu yote ingewekwa kwenye mizani! 1
3Kwa kuwa hakika ingekuwa nzito kuliko mchanga wa bahari zote, 2 kwa hiyo si ajabu maneno yangu yamekuwa ya haraka. 1
4Mishale ya Mwenyezi iko ndani yangu, 2 roho yangu inakunywa sumu yake; 2 vitisho vya Mungu vimejipanga dhidi yangu. 1
5Je, punda-mwitu hulia akiwa na majani, 2 au ngʼombe dume hulia akiwa na chakula? 1
6Je, chakula kisicho na ladha huliwa bila chumvi, 2 au upo utamu katika ute mweupe wa yai? 1
7Ninakataa kuvigusa; 2 vyakula vya aina hii hunichukiza. 1
8“Laiti ningepata haja yangu, 2 kwamba Mungu angenijalia hilo nililotarajia, 1
9kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda, 2 kuuachia mkono wake na kunikatilia mbali! 1
10Ndipo bado ningekuwa na hii faraja, 2 furaha yangu katika maumivu makali: 2 kwamba sikuwa nimeyakana maneno yake yeye Aliye Mtakatifu. 1
11“Ninazo nguvu gani, hata niendelee kutumaini? 2 Matazamio yangu ya mbele ni nini, hata niendelee kuwa mvumilivu? 1
12Je, mimi nina nguvu za jiwe? 2 Je, mwili wangu ni shaba? 1
13Je, ninao uwezo wowote wa kujisaidia mimi mwenyewe, 2 wakati ambapo mafanikio yamefukuziwa mbali nami? 1
14“Mtu anayekata tamaa angetazamia moyo wa kujitoa wa rafiki zake, 2 hata kama akiacha uchaji wa Mwenyezi. 1
15Lakini ndugu zangu sio wa kutegemewa, 2 ni kama vijito vya msimu, 2 ni kama vijito ambavyo hufurika 1
16wakati vimefunikwa barafu iyeyukayo, 2 ambavyo hujazwa na theluji inayoyeyuka, 1
17lakini hukauka majira ya ukame, 2 na wakati wa hari hutoweka katika mikondo yake. 1
18Misafara hugeuka kutoka njia zake; 2 hukwea kwenda kwenye nchi ya ukiwa na kuangamia. 1
19Misafara ya Tema inatafuta maji, 2 wafanyabiashara wa Sheba wanaosafiri 2 hutazama kwa matarajio. 1
20Wamedhikika, kwa sababu walikuwa na matumaini; 2 wanafika huko, lakini wanahuzunika kwa kukosa walichotarajia. 1
21Sasa nanyi mmethibitika kwamba hamna msaada wowote; 2 mnaona jambo la kutisha, nanyi mnaogopa. 1
22Je, nimewahi kusema, ‘Toeni kitu kwa ajili yangu, 2 au mnilipie fidia kutoka mali zenu, 1
23au niokoeni mikononi mwa adui, 2 au nikomboeni kutoka makucha ya wasio na huruma’? 1
24“Nifundisheni, nami nitanyamaza kimya; 2 nionyesheni nilikokosea. 1
25Tazama yalivyo ya kuumiza maneno ya kweli! 2 Lakini mabishano yenu yanathibitisha nini? 1
26Je, mna maana ya kuyasahihisha ninayosema, 2 na kuyafanya maneno ya mtu anayekata tamaa kama upepo? 1
27Mngeweza hata kupiga kura kwa ajili ya yatima, 2 na kubadilishana rafiki yenu na mali. 1
28“Lakini sasa kuweni na huruma mkaniangalie mimi. 2 Je, ningeweza kusema uongo mbele zenu? 1
29Tulizeni hasira, msiwe wadhalimu; 2 angalieni tena, kwa maana nimehatarisha uadilifu wangu. + 6:29 Au: haki yangu bado inasimama. 1
30Je, pana uovu wowote midomoni mwangu? 2 Je, kinywa changu hakiwezi kupambanua hila?