Job · Biblia (Kiswahili)

Job 5

1“Ita kama unataka, lakini ni nani atakayekujibu? 2 Ni yupi kati ya hao watakatifu utakayemgeukia? 1

2Kuweka uchungu moyoni humuua mpumbavu, 2 nao wivu humchinja mjinga. 1

3Mimi mwenyewe nimemwona mpumbavu akistawi, 2 lakini ghafula nyumba yake ikawa imelaaniwa. 1

4Watoto wake wako mbali na usalama, 2 hushindwa mahakamani bila mtetezi. 1

5Wenye njaa huyala mavuno yake, 2 wakiyatoa hata katikati ya miiba, 2 nao wenye kiu huitamani sana mali yake. 1

6Kwa maana taabu haioti kutoka kwenye udongo, 2 wala udhia hauchipui kutoka ardhini. 1

7Lakini mwanadamu huzaliwa ili kutaabika, 2 kwa hakika kama cheche za moto zirukavyo kuelekea juu. 1

8“Lakini ingekuwa ni mimi, ningemlalamikia Mungu, 2 ningeliweka shauri langu mbele zake. 1

9Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa, 2 miujiza isiyoweza kuhesabika. 1

10Yeye huipa nchi mvua, 2 huyapeleka maji kunyesha mashamba. 1

11Huwainua juu wanyonge, 2 nao wale waombolezao huinuliwa wakawa salama. 1

12Huipinga mipango ya wenye hila, 2 ili mikono yao isifikie ufanisi. 1

13Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao, 2 nayo mipango ya wadanganyifu huifagilia mbali. 1

14Giza huwapata wakati wa mchana; 2 wakati wa adhuhuri hupapasa kama vile usiku. 1

15Humwokoa mhitaji kutokana na upanga ulioko kinywani mwao; 2 huwaokoa kutokana na makucha ya wenye nguvu. 1

16Kwa hiyo maskini analo tarajio, 2 nao udhalimu hufumba kinywa chake. 1

17“Heri mtu yule ambaye Mungu humrudi; 2 kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi. + 5:17 Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania Shaddai (hapa na kila mahali katika kitabu hiki cha Ayubu). 1

18Kwa kuwa hutia jeraha, lakini pia huyafunga; 2 huumiza, lakini mikono yake pia huponya. 1

19Kutoka majanga sita atakuokoa; 2 naam, hata katika saba hakuna dhara litakalokupata wewe. 1

20Wakati wa njaa atakukomboa wewe na kifo, 2 naye katika vita atakukomboa na pigo la upanga. 1

21Utalindwa kutokana na kichapo cha ulimi, 2 wala hutakuwa na sababu ya kuogopa maangamizi yatakapokujia. 1

22Utayacheka maangamizo na njaa, 2 wala hutakuwa na sababu ya kuwaogopa 2 wanyama wakali wa mwituni. 1

23Kwa kuwa utakuwa na agano na mawe ya mashamba, 2 nao wanyama wa mwitu watakuwa na amani nawe. 1

24Utajua ya kwamba hema lako li salama; 2 utahesabu mali zako wala hutakuta chochote kilichopungua. 1

25Utajua ya kuwa watoto wako watakuwa wengi, 2 nao wazao wako wengi kama majani ya nchi. 1

26Utaingia kaburini ukiwa na umri wa uzee mtimilifu, 2 kama masuke ya ngano yakusanywapo kwa wakati wake. 1

27“Tumelichunguza hili, nalo ni kweli. 2 Hivyo lisikie na ulitendee kazi.”

← Job 4Read In The App, Free →Job 6 →

Study Job 5

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142