Job 29
1Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema: 1
2“Tazama jinsi ninavyoitamani miezi iliyopita, 2 zile siku ambazo Mungu alikuwa akinilinda, 1
3wakati taa yake iliniangazia kichwani changu, 2 na kwa mwanga wake Mungu nikapita katikati ya giza! 1
4Natamani siku zile nilizokuwa katika ustawi wangu, 2 wakati urafiki wa Mungu wa ndani ulipoibariki nyumba yangu, 1
5wakati Mwenyezi alikuwa pamoja nami, 2 nao watoto wangu walikuwa wamenizunguka, 1
6wakati njia yangu ilikuwa imenyweshewa siagi, 2 nao mwamba ukanimiminia vijito vya mafuta ya zeituni. 1
7“Wakati nilipokwenda kwenye lango la mji 2 na kuketi katika kiwanja, 1
8vijana waliniona wakakaa kando, 2 nao wazee walioketi wakasimama; 1
9wakuu wakaacha kuzungumza 2 na kuziba vinywa vyao kwa mikono yao; 1
10wenye vyeo wakanyamazishwa, 2 nazo ndimi zao zikagandamana na makaakaa ya vinywa vyao. 1
11Yeyote aliyenisikia alinena mema juu yangu, 2 nao walioniona walinisifu, 1
12kwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada, 2 naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia. 1
13Mtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki, 2 nami niliufanya moyo wa mjane kuimba. 1
14Niliivaa haki kama vazi langu; 2 uadilifu ulikuwa joho langu na kilemba changu. 1
15Nilikuwa macho ya kipofu 2 na miguu kwa kiwete. 1
16Nilikuwa baba kwa mhitaji; 2 nilimtetea mgeni. 1
17Niliyavunja meno makali ya waovu, 2 na kuwapokonya wahanga kwenye meno yao. 1
18“Nikafikiri, ‘Nitafia katika nyumba yangu mwenyewe, 2 nazo siku zangu zitakuwa nyingi kama chembechembe za mchanga. 1
19Mizizi yangu itafika mpaka kwenye maji, 2 nao umande utakaa juu ya matawi yangu usiku kucha. 1
20Utukufu wangu utabakia kuwa mpya ndani yangu, 2 upinde wangu daima utaendelea kuwa mpya mkononi mwangu.’ 1
21“Watu walinisikiliza kwa tumaini, 2 wakingojea ushauri wangu kwa utulivu. 1
22Baada ya mimi kuzungumza, hawakusema zaidi; 2 maneno yangu yaliingia masikioni mwao kwa makini. 1
23Waliningojea kama manyunyu ya mvua 2 na kuyapokea maneno yangu 2 kama ardhi inyonyavyo mvua ya vuli. 1
24Walipokata tamaa niliwaonyesha uso wa furaha; 2 nuru ya uso wangu ilikuwa ya thamani kwao. 1
25Niliwachagulia njia na kukaa kama mkuu wao; 2 niliishi kama mfalme katikati ya majeshi yake; 2 nikawa kama yeye anayewafariji waombolezaji.