Job · Biblia (Kiswahili)

Job 31

1“Nimefanya agano na macho yangu 2 yasimtazame msichana kwa kumtamani. 1

2Kwa kuwa fungu la mwanadamu ni gani kutoka kwa Mungu juu, 1 urithi wake kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu Aliye juu? 1

3Je, si uharibifu kwa watu waovu, 2 maangamizi kwa wale watendao mabaya? 1

4Je, yeye hazioni njia zangu 2 na kuihesabu kila hatua yangu? 1

5“Kama nimeishi katika uongo 2 au mguu wangu umekimbilia udanganyifu, 1

6Mungu na anipime katika mizani za uaminifu, 2 naye atajua kwamba sina hatia: 1

7kama hatua zangu zimepotoka kutoka kwenye njia, 2 kama moyo wangu umeongozwa na macho yangu, 2 au kama mikono yangu imetiwa unajisi, 1

8basi wengine na wale nilichokipanda, 2 nayo yale yote niliyootesha na yangʼolewe. 1

9“Kama moyo wangu umeshawishiwa na mwanamke, 2 au kama nimevizia mlangoni mwa jirani yangu, 1

10basi mke wangu na asage nafaka ya mwanaume mwingine, 2 nao wanaume wengine walale naye. 1

11Kwa kuwa hilo lingekuwa aibu, 2 naam, dhambi ya kuhukumiwa. 1

12Ni moto uwakao kwa Uharibifu; + 31:12 Kwa Kiebrania ni Abadon ( Ay 26:6; Mit 15:11 ). 2 ungekuwa umengʼoa mavuno yangu. 1

13“Kama ningewanyima haki watumishi wangu wanaume au vijakazi wangu, 2 walipokuwa na manungʼuniko dhidi yangu, 1

14nitafanya nini Mungu atakaponikabili? 2 Nitamjibu nini nitakapoitwa kutoa hesabu? 1

15Je, yeye aliyeniumba tumboni mwa mama yangu, 2 si ndiye aliwaumba? 1 Je, si ni yeye huyo mmoja aliyetuumba sote 2 ndani ya mama zetu? 1

16“Ikiwa nimewanyima maskini haja zao, 2 au kuyaacha macho ya wajane yadhoofike, 1

17kama nimekula chakula changu mwenyewe, 2 bila kuwashirikisha yatima; 1

18lakini tangu ujana wangu nimemlea yatima kama ambavyo baba angefanya, 2 nami tangu kuzaliwa kwangu nimewaongoza wajane: 1

19kama nilimwona yeyote akiteseka kwa kukosa nguo, 2 au mtu mhitaji asiye na mavazi 1

20ambaye wala moyo wake haukunibariki 2 kwa kumpatia joto kwa mavazi ya manyoya ya kondoo zangu, 1

21na kama nimeinua mkono wangu dhidi ya yatima, 2 nikijua kuwa nina ushawishi mahakamani, 1

22basi mkono wangu na unyofoke toka begani mwangu, 2 nao na uvunjike kutoka kiungio chake. 1

23Kwa kuwa niliogopa uharibifu kutoka kwa Mungu, 2 nami kwa kuuogopa utukufu wake sikuweza kufanya mambo kama hayo. 1

24“Kama nimeweka tumaini langu kwenye dhahabu, 2 au kuiambia dhahabu safi, ‘Wewe ndiwe salama yangu,’ 1

25kama nimefurahia wingi wa utajiri wangu, 2 ustawi ambao mikono yangu ilikuwa imepata, 1

26kama nimelitazama jua katika kungʼaa kwake 2 au mwezi ukienda kwa fahari yake, 1

27hivyo moyo wangu kushawishiwa kwa siri, 2 au kubusu mkono wangu kwa kuviheshimu, 1

28basi hiyo pia ingekuwa dhambi ya kuhukumiwa, 2 kwa kuwa ningekuwa si mwaminifu kwa Mungu aishiye juu sana. 1

29“Kama nimeshangilia msiba wa adui yangu, 2 au kutazama kwa furaha taabu iliyomjia, 1

30lakini sikuruhusu kinywa changu kufanya dhambi 2 kwa kuomba laana dhidi ya maisha yake; 1

31kama watu wa nyumbani mwangu kamwe hawakusema, 2 ‘Ni nani ambaye hajashibishwa na nyama ya Ayubu?’ 1

32Lakini hakuna mgeni aliyelala njiani, 2 kwa maana mlango wangu ulikuwa wazi kwa msafiri; 1

33kama nimeifunika dhambi yangu kama wanadamu wengine wafanyavyo, 2 kwa kuficha hatia yangu moyoni mwangu, 1

34kwa sababu ya kuogopa umati wa watu, 2 na hivyo kuwa na hofu ya kudharauliwa na jamaa, 2 nikanyamaza kimya nisitoke nje ya mlango: 1

35(“Laiti kama angekuwepo mtu wa kunisikia! 2 Tazama sasa ninatia sahihi kwenye utetezi wangu: 2 Mwenyezi na anijibu; 1 mshtaki wangu na aweke mashtaka yake kwenye maandishi. 1

36Hakika ningeyavaa begani mwangu, 2 ningeyavaa kama taji. 1

37Ningempa hesabu ya kila hatua yangu, 2 ningemwendea kama mwana wa mfalme.) 1

38“Kama nchi yangu inalia dhidi yangu, 2 na mifereji yake yote imelowana kwa machozi, 1

39kama nimekula mazao yake bila malipo, 2 au kuvunja mioyo ya wapangaji wake, 1

40basi miiba na iote badala ya ngano, 2 na magugu badala ya shayiri.” Mwisho wa maneno ya Ayubu.

← Job 30Read In The App, Free →Job 32 →

Study Job 31

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142