Job · Biblia (Kiswahili)

Job 39

1“Je, wajua ni wakati gani mbuzi wa mlimani wanapozaa? 2 Je, watambua ni wakati gani kulungu jike azaapo mtoto wake? 1

2Je, waweza kuhesabu miezi hadi wazaapo? 2 Je, unajua majira yao ya kuzaa? 1

3Wao hujiinamisha na kuzaa watoto wao; 2 utungu wa kuzaa unakoma. 1

4Watoto wao hustawi na kuongezeka nguvu nyikani; 2 huenda zao wala hawarudi tena. 1

5“Ni nani aliyemwachia punda-mwitu awe huru? 2 Ni nani aliyezifungua kamba zake? 1

6Nimempa nchi isiyokaliwa na watu kuwa masikani yake, 2 nchi ya chumvi kuwa makao yake. 1

7Huzicheka ghasia za mji, 2 wala hasikii kelele za mwendesha gari. 1

8Huzunguka vilimani kwa ajili ya malisho 2 na kutafuta kila kitu kibichi. 1

9“Je, nyati atakubali kukutumikia? 2 Atakaa karibu na hori lako usiku? 1

10Je, waweza kumfungia kwenye matuta kwa kamba? 2 Je, atalima mabonde nyuma yako? 1

11Je, utamtumainia kwa ajili ya nguvu zake nyingi? 2 Utamwachia yeye kazi zako nzito? 1

12Utaweza kumwamini akuletee nafaka yako nyumbani 2 kutoka shambani na kuikusanya kwenye sakafu yako ya kupuria? 1

13“Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa furaha, 2 lakini hayawezi kulinganishwa 2 na mabawa na manyoya ya korongo. 1

14Huyataga mayai yake juu ya ardhi, 2 na kuyaacha yapate joto mchangani, 1

15bila kujali kuwa mguu waweza kuyaponda, 2 kwamba baadhi ya wanyama wa porini wanaweza kuyakanyaga. 1

16Yeye huyafanyia makinda yake ukatili kama vile si yake; 2 hajali kwamba taabu yake inaweza ikawa bure, 1

17kwa kuwa Mungu hakumjalia hekima, 2 wala hakumpa fungu la akili njema. 1

18Lakini akunjuapo mabawa yake kukimbia, 2 humcheka farasi pamoja na yeye aliyempanda. 1

19“Je, wewe humpa farasi nguvu 2 au kuivika shingo yake manyoya marefu? 1

20Je, wewe humfanya farasi aruke kama nzige, 2 akistaajabisha kwa tishio la mlio wake wa majivuno? 1

21Huparapara bila woga, akizifurahia nguvu zake, 2 husonga mbele kukabiliana na silaha. 1

22Huicheka hofu, haogopi chochote, 2 wala haukimbii upanga. 1

23Podo hutoa sauti kando yake, 2 pamoja na mkuki unaongʼaa na fumo. 1

24Bila woga na kwa ghadhabu huimeza nchi, 2 wala tarumbeta iliapo yeye hawezi kusimama. 1

25Asikiapo sauti ya baragumu yeye hulia, ‘Aha!’ 2 Hunusa harufu ya vita toka mbali, 2 sauti ya mtoa amri na ukelele wa vita. 1

26“Je, mwewe huruka kwa hekima yako 2 na kuyakunjua mabawa yake kuelekea kusini? 1

27Je, tai hupaa juu kwa amri yako 2 na kujenga kiota chake mahali pa juu? 1

28Huishi juu ya miamba mirefu na kukaa huko usiku; 2 majabali yenye ncha kali ndiyo ngome yake. 1

29Kutoka huko hutafuta chakula chake; 2 macho yake hukiona kutoka mbali. 1

30Makinda yake hujilisha damu, 2 na pale palipo na machinjo, ndipo yeye alipo.”

← Job 38Read In The App, Free →Job 40 →

Study Job 39

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142