Job · Biblia (Kiswahili)

Job 20

1Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu: 1

2“Mawazo yanayonisumbua yananisukuma kujibu, 2 kwa sababu nimehangaika sana. 1

3Ninasikia makaripio ambayo yananivunjia heshima, 2 nao ufahamu wangu unanisukuma kujibu. 1

4“Hakika unajua jinsi ilivyokuwa tangu zamani, 2 tangu zamani mwanadamu alipowekwa duniani, 1

5macheko ya mtu mwovu ni ya muda mfupi, 2 nayo furaha ya wasiomcha Mungu hudumu kwa kitambo tu. 1

6Ingawa kujikweza kwake hufikia mbinguni 2 na kichwa chake hugusa mawingu, 1

7ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe. 2 Wale waliomwona watauliza, ‘Yuko wapi?’ 1

8Kama ndoto hutoweka, wala hapatikani tena, 2 amefukuziwa mbali kama maono ya usiku. 1

9Jicho lililomwona halitamwona tena; 2 mahali pake hapatamwona tena. 1

10Watoto wake watalipa yote baba yao aliyowadhulumu maskini, 2 nayo mikono yake itarudisha mali yote aliyonyangʼanya watu. 1

11Nguvu za ujana zilizoijaza mifupa yake, 2 zitalala naye mavumbini. 1

12“Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake 2 naye huuficha chini ya ulimi wake, 1

13ingawa hawezi kukubali kuuachia uende, 2 lakini huuweka kinywani mwake. 1

14Hata hivyo chakula chake kitakuwa kichungu tumboni mwake, 2 nacho kitakuwa sumu kali ya nyoka ndani yake. 1

15Atatema mali alizozimeza; 2 Mungu atalifanya tumbo lake kuzitapika. 1

16Atanyonya sumu za majoka; 2 meno ya nyoka mwenye sumu kali yatamuua. 1

17Hatafurahia vijito, 2 mito inayotiririsha asali na siagi. 1

18Vile alivyovitaabikia atavirudisha bila kuvila; 2 hatafurahia faida itokanayo na biashara yake. 1

19Kwa kuwa aliwaonea maskini na kuwaacha pasipo kitu; 2 amenyangʼanya kwa nguvu nyumba asizozijenga. 1

20“Hakika hatakuwa na raha katika kutamani kwake sana; 2 hawezi kujiokoa mwenyewe kwa hazina zake. 1

21Hakuna chochote kitakachosalia kwa ajili yake ili ale; 2 kufanikiwa kwake hakutadumu. 1

22Katikati ya wingi wa ustawi wake, dhiki itampata; 2 taabu itamjia kwa nguvu zote. 1

23Atakapokuwa amelijaza tumbo lake, 2 Mungu ataionyesha ghadhabu kali dhidi yake, 2 na kumnyeshea mapigo juu yake. 1

24Ijapokuwa aikimbia silaha ya chuma, 2 mshale wa shaba utamchoma. 1

25Atauchomoa katika mgongo wake, 2 ncha ingʼaayo kutoka ini lake. 1 Vitisho vitakuja juu yake; 2

26giza nene linavizia hazina zake. 1 Moto usiopepewa na mtu utamteketeza, 2 na kuangamiza yaliyosalia nyumbani mwake. 1

27Mbingu zitaweka wazi hatia yake, 2 nayo nchi itainuka kinyume chake. 1

28Mafuriko yataichukua nyumba yake, 2 maji yaendayo kasi katika siku ya ghadhabu ya Mungu. 1

29Hili ndilo fungu Mungu alilowagawia waovu, 2 urithi uliowekwa kwa ajili yao na Mungu.”

← Job 19Read In The App, Free →Job 21 →

Study Job 20

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142