Job · Biblia (Kiswahili)

Job 33

1“Lakini Ayubu, sasa, sikiliza maneno yangu; 2 zingatia kila kitu nitakachosema. 1

2Karibu nitafungua kinywa changu; 2 maneno yangu yapo katika ncha ya ulimi wangu. 1

3Maneno yangu yanatoka katika moyo mnyofu; 2 midomo yangu hunena kwa uaminifu yale niyajuayo. 1

4Roho wa Mungu ameniumba; 2 pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai. 1

5Unijibu basi, kama unaweza; 2 jiandae kunikabili mimi. 1

6Mimi ni kama wewe mbele za Mungu; 2 mimi pia nimetolewa kwenye udongo. 1

7Huna sababu ya kuniogopa, 2 wala mkono wangu haupaswi kukulemea. 1

8“Lakini umesema nikiwa ninakusikia, 2 nami nilisikia maneno yenyewe: 1

9‘Mimi ni safi na sina dhambi; 2 mimi ni safi na sina hatia. 1

10Lakini bado Mungu amepata dosari kwangu, 2 naye ananiona kama adui yake. 1

11Ananifunga miguu kwa pingu, 2 tena anaziangalia njia zangu zote kwa karibu.’ 1

12“Lakini mimi ninakuambia, katika jambo hili wewe una makosa, 2 kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu. 1

13Kwa nini unamlalamikia 2 kwamba yeye hamjibu mwanadamu? 1

14Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja, 2 au wakati mwingine kwa njia nyingine, 2 ingawa mwanadamu anaweza asielewe. 1

15Mungu husema na mwanadamu katika ndoto, 2 katika maono ya usiku, 1 wakati usingizi mzito uwaangukiapo 2 wanadamu wasinziapo vitandani mwao, 1

16anaweza akasemea masikioni mwao, 2 na kuwatia hofu kwa maonyo, 1

17ili kumgeuza mtu kutoka kwenye kutenda mabaya 2 na kumwepusha na kiburi, 1

18kuiokoa nafsi yake na shimo, 2 uhai wake usiangamizwe kwa upanga. 1

19Mtu anaweza kutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, 2 kwa dhiki za mfululizo katika mifupa yake, 1

20kiasi kwamba maisha yake yenyewe yanakataa chakula 2 nayo nafsi yake ikakichukia kabisa hata chakula kizuri. 1

21Nyama ya mwili wake huisha kwa kukonda, 2 nayo mifupa yake ambayo mwanzoni ilikuwa imefichika, 2 sasa inatokeza nje. 1

22Nafsi yake inakaribia kaburi, 2 nao uhai wake karibu na wajumbe wa kifo. 1

23“Kama bado kuna malaika upande wake 2 kama mtetezi, mmoja miongoni mwa elfu, 2 wa kumwambia mwanadamu lililo jema kwake, 1

24kumwonea huruma na kusema, 2 ‘Mwokoe asije akatumbukia shimoni; 2 nimepata ukombozi kwa ajili yake’: 1

25ndipo nyama ya mwili wake hufanywa mpya kama ya mtoto; 2 hurudishwa upya kama siku za ujana wake. 1

26Humwomba Mungu, akapata kibali kwake, 2 huuona uso wa Mungu na kushangilia kwa furaha; 2 Mungu humrudisha katika hali yake ya uadilifu. 1

27Ndipo huja mbele za watu na kusema, 2 ‘Nilitenda dhambi na kupotosha kilichokuwa haki, 2 lakini sikuadhibiwa kama nilivyostahili. 1

28Alinikomboa nafsi yangu nisitumbukie shimoni, 2 nami nitaishi ili kuufurahia mwanga.’ 1

29“Mungu hufanya haya yote kwa mwanadamu; 2 mara mbili hata mara tatu, 1

30ili aigeuze nafsi yake toka shimoni, 2 ili nuru ya uzima imwangazie. 1

31“Ayubu, zingatia, nisikilize mimi; 2 nyamaza, nami nitanena. 1

32Kama unalo lolote la kusema, unijibu; 2 sema, kwa maana ninataka uonekane huna hatia. 1

33Lakini kama huna la kusema, basi nisikilize mimi; 2 nyamaza, nami nitakufundisha hekima.”

← Job 32Read In The App, Free →Job 34 →

Study Job 33

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142