Job · Biblia (Kiswahili)

Job 16

1Kisha Ayubu akajibu: 1

2“Nimepata kusikia mambo mengi kama haya, 2 nanyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha! 1

3Je, maneno yenu mengi yasiyo na maana hayana mwisho? 2 Mna nini hata mwendelee kushindana kwa maneno? 1

4Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi, 2 kama mngekuwa katika hali yangu; 1 ningeweza kutoa hotuba nzuri dhidi yenu, 2 na kuwatikisia ninyi kichwa changu. 1

5Lakini kinywa changu kingewatia moyo; 2 faraja kutoka midomoni mwangu, ingewaletea nafuu. 1

6“Lakini kama nikisema, maumivu yangu bado hayatulizwi; 2 nami kama nikijizuia, wala hayaondoki. 1

7Ee Mungu, hakika umenichakaza; 2 umewaangamiza kabisa watu wa nyumbani mwangu wote. 1

8Umenikunjakunja, nalo limekuwa ushahidi; 2 nako kukonda kwangu kumeongezeka sana na kushuhudia dhidi yangu. 1

9Mungu amenishambulia na kunirarua katika hasira yake, 2 na kunisagia meno yake; 2 adui yangu hunikazia macho yake makali. 1

10Watu wamenifumbulia vinywa vyao kunidhihaki; 2 hunipiga shavuni mwangu kwa dharau, 2 na kuungana pamoja dhidi yangu. 1

11Mungu amenigeuzia kwa watu wabaya, 2 na kunitupa katika makucha ya waovu. 1

12Mambo yote yalikuwa mazuri, lakini alinivunjavunja; 2 amenikamata shingo na kuniponda. 2 Amenifanya mimi kuwa shabaha yake; 1

13wapiga upinde wake wananizunguka. 2 Bila huruma, huchoma figo zangu, 2 na kuimwaga nyongo yangu juu ya nchi. 1

14Huniponda tena na tena; 2 hunishambulia kama shujaa wa vita. 1

15“Nimejishonea nguo ya gunia juu ya mwili wangu 2 nami nimekizika kipaji cha uso wangu kwenye vumbi. 1

16Uso wangu umekuwa mwekundu kwa kulia, 2 macho yangu yamepigwa na giza kuu. 1

17Hata hivyo mikono yangu haijafanya jeuri, 2 na maombi yangu ni safi. 1

18“Ee nchi, usiifunike damu yangu, 2 nacho kilio changu kisinyamazishwe kamwe. 1

19Hata sasa shahidi wangu yuko mbinguni; 2 wakili wangu yuko juu. 1

20Mwombezi wangu ni rafiki yangu 2 macho yangu yamwagapo machozi kwa Mungu; 1

21kwa niaba ya mtu anamsihi Mungu 2 kama mtu anavyosihi kwa ajili ya rafiki yake. 1

22“Ni miaka michache tu itapita 2 kabla sijaenda safari ambayo sitarudi.

← Job 15Read In The App, Free →Job 17 →

Study Job 16

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142