Job · Biblia (Kiswahili)

Job 19

1Ndipo Ayubu akajibu: 1

2“Je, mtaendelea kunitesa mpaka lini, 2 na kuniponda kwa maneno yenu? 1

3Mara kumi hizi mmenishutumu; 2 bila aibu mnanishambulia. 1

4Kama ni kweli nimepotoka, 2 kosa langu ninabaki kuhusika nalo mwenyewe. 1

5Kama kweli mngejitukuza wenyewe juu yangu, 2 na kutumia unyonge wangu dhidi yangu, 1

6basi jueni kuwa Mungu amenitendea yaliyo mabaya, 2 naye amekokota wavu wake kunizunguka. 1

7“Ingawa ninalia, ‘Nimetendewa mabaya!’ sipati jibu; 2 ingawa ninaomba msaada, hakuna haki. 1

8Yeye ameizuia njia yangu hivyo siwezi kupita; 2 ameyafunika mapito yangu na giza. 1

9Amenivua heshima yangu, 2 na kuniondolea taji kichwani pangu. 1

10Amenibomoa kila upande hadi nimeisha; 2 amelingʼoa tegemeo langu kama mti. 1

11Hasira yake imewaka juu yangu; 2 amenihesabu kuwa miongoni mwa adui zake. 1

12Majeshi yake yananisogelea kwa nguvu; 2 yamenizingira, 2 yamepiga kambi kulizunguka hema langu. 1

13“Amewatenga ndugu zangu mbali nami; 2 wale tunaojuana nao wamefarakana nami kabisa. 1

14Watu wa jamaa yangu wamekwenda mbali; 2 rafiki zangu wamenisahau. 1

15Wageni wangu na watumishi wangu wa kike wananiona kama mgeni; 2 wananitazama kama mgeni. 1

16Namwita mtumishi wangu, wala haitiki, 2 ingawa namwomba kwa kinywa changu mwenyewe. 1

17Pumzi ya kinywa changu ni kinyaa kwa mke wangu; 2 nimekuwa chukizo mno kwa ndugu zangu mwenyewe. 1

18Hata watoto wadogo hunidhihaki; 2 ninapojitokeza, hunifanyia mzaha. 1

19Rafiki zangu wa moyoni wote wananichukia kabisa; 2 wale niwapendao wamekuwa kinyume nami. 1

20Mimi nimebaki mifupa na ngozi tu; 2 nimeponea nikiwa karibu kufa. 1

21“Nihurumieni, rafiki zangu, kuweni na huruma, 2 kwa kuwa mkono wa Mungu umenipiga. 1

22Kwa nini mnanifuatia kama Mungu afanyavyo? 2 Hamtosheki kamwe na mwili wangu? 1

23“Laiti maneno yangu yangewekwa kwenye kumbukumbu, 2 laiti kwamba yangeandikwa kwenye kitabu, 1

24kwamba yangechorwa kwenye risasi kwa kifaa cha chuma, 2 au kuyachonga juu ya mwamba milele! 1

25Ninajua kwamba Mkombozi + 19:25 Au: Mtetezi. wangu yu hai, 2 naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi. 1

26Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa, 2 bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu; 1

27mimi nitamwona kwa macho yangu mwenyewe: 2 mimi, wala si mwingine. 2 Tazama jinsi moyo wangu unavyomtamani sana! 1

28“Kama mkisema, ‘Tazama tutakavyomwinda, 2 maadamu mzizi wa tatizo uko ndani yake,’ 1

29ninyi wenyewe uogopeni upanga, 2 kwa kuwa ghadhabu italeta adhabu kwa upanga, 2 nanyi ndipo mtakapojua kwamba kuna hukumu.”

← Job 18Read In The App, Free →Job 20 →

Study Job 19

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142