Job 28
1“Kuna machimbo ya fedha, 2 na mahali dhahabu isafishwapo. 1
2Chuma hupatikana ardhini, 2 nayo shaba huyeyushwa kutoka mawe ya madini. 1
3Mwanadamu hukomesha giza; 2 huyatafuta hadi sehemu iliyo mbali, 1 kwa ajili ya kuchimbua mawe yenye madini 2 katika giza jeusi sana. 1
4Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu, 2 mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu; 2 mbali na wanadamu huningʼinia na kupembea kwa kamba. 1
5Ardhi, ambako chakula hutoka, 2 chini hugeuzwa kwa moto; 1
6yakuti samawi hutoka katika miamba yake, 2 nalo vumbi lake lina vipande vya dhahabu. 1
7Hakuna ndege awindaye aijuaye njia ile iliyofichika, 2 wala hakuna jicho la mwewe lililoiona. 1
8Wanyama wa porini wanaotamba hawajawahi kupakanyaga, 2 wala simba azungukaye huko. 1
9Mikono ya mwanadamu hushambulia miamba migumu sana, 2 na kuiacha wazi mizizi ya milima. 1
10Hutoboa shimo refu la kupenya chini kwa chini kwenye miamba; 2 macho yake huona hazina zake zote. 1
11Hutafuta vyanzo vya mito 2 na kuvileta vitu vilivyofichika katika nuru. 1
12“Lakini hekima inaweza kupatikana wapi? 2 Ufahamu unakaa wapi? 1
13Mwanadamu hatambui thamani yake; 2 haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai. 1
14Kilindi husema, ‘Haiko ndani yangu’; 2 bahari nayo husema, ‘Haiko pamoja nami.’ 1
15Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi kuliko zote, 2 wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha. 1
16Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu ya Ofiri, 2 kwa shohamu ya thamani kubwa au yakuti samawi ya thamani kubwa. 1
17Dhahabu wala mawe maangavu haviwezi kulinganishwa nayo, 2 wala haiwezi hubadilishwa na vito vya dhahabu. 1
18Marijani na yaspi hazistahili kutajwa; 2 thamani ya hekima ni zaidi ya akiki nyekundu. 1
19Yakuti manjano ipatikanayo Kushi haiwezi kulinganishwa nayo, 2 wala haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi. 1
20“Ni wapi basi hekima itokako? 2 Ufahamu hukaa wapi? 1
21Imefichika machoni pa kila kitu kilicho hai, 2 imesitiriwa hata kwa ndege wa angani. 1
22Uharibifu na Mauti husema, 2 ‘Ni uvumi wake tu uliotufikia masikioni mwetu.’ 1
23Mungu anaifahamu njia ya kuiendea hekima 2 na ndiye peke yake anayefahamu inakokaa, 1
24kwa maana yeye huitazama miisho ya dunia 2 na huona kila kitu chini ya mbingu. 1
25Alipofanyiza nguvu za upepo 2 na kuyapima maji, 1
26alipofanya maagizo kwa ajili ya mvua 2 na njia kwa ajili ya umeme wa radi, 1
27ndipo alipoitazama hekima na kuikadiria thamani yake, 2 akaithibitisha na kuihakikisha. 1
28Naye Mungu akamwambia mwanadamu, 2 ‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima, 2 nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ ”