Job · Biblia (Kiswahili)

Job 26

1Kisha Ayubu akajibu: 1

2“Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo! 2 Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu! 1

3Ni shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima? 2 Nayo ni busara gani kubwa uliyoonyesha! 1

4Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo? 2 Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako? 1

5“Wafu wako katika maumivu makuu, 2 wale walio chini ya maji na wale waishio ndani yake. 1

6Mauti + 26:6 Yaani Kuzimu; Kiebrania ni Sheol. iko wazi mbele za Mungu; 2 Uharibifu + 26:6 Kwa Kiebrania ni Abadon. haukufunikwa. 1

7Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu; 2 naye huiningʼiniza dunia mahali pasipo na kitu. 1

8Huyafungia maji kwenye mawingu yake, 2 hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake. 1

9Huufunika uso wa mwezi mpevu, 2 akitandaza mawingu juu yake. 1

10Amechora mstari wa upeo juu ya uso wa maji, 2 ameweka mpaka wa nuru na giza. 1

11Nguzo za mbingu nazo zatetemeka, 2 zinatishika anapozikemea. 1

12Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari; 2 kwa hekima yake alimkata Rahabu + 26:12 Rahabu hapa ni fumbo la kumaanisha Lewiathani, mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. vipande vipande. 1

13Aliisafisha anga kwa pumzi yake; 2 kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio. 1

14Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake; 2 tazama jinsi ulivyo mdogo mnongʼono tunaousikia kumhusu! 1 Ni nani basi awezaye kuelewa 2 ngurumo za nguvu zake?”

← Job 25Read In The App, Free →Job 27 →

Study Job 26

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142