Job · Biblia (Kiswahili)

Job 4

1Ndipo Elifazi Mtemani akajibu: 1

2“Kama mtu akithubutu kuzungumza nawe, 2 kutakukasirisha? 1 Lakini ni nani awezaye 2 kujizuia asiseme? 1

3Fikiri jinsi ambavyo umewafundisha watu wengi, 2 jinsi ambavyo umeitia nguvu 2 mikono iliyokuwa dhaifu. 1

4Maneno yako yamewategemeza wale waliojikwaa; 2 umeyatia nguvu magoti yaliyokuwa dhaifu. 1

5Lakini sasa hii taabu imekujia wewe, 2 nawe unashuka moyo; 1 imekupiga wewe, 2 nawe unafadhaika. 1

6Je, kumcha Mungu kwako hakupaswi kuwa 2 ndiyo matumaini yako 1 na njia zako kutokuwa na lawama 2 ndilo taraja lako? 1

7“Fikiri sasa: Ni mtu yupi asiye na hatia ambaye aliwahi kuangamia? 2 Ni wapi wanyofu waliwahi kuangamizwa? 1

8Kwa jinsi ambavyo mimi nimechunguza, 2 wale walimao ubaya 1 na wale hupanda uovu, 2 huvuna hayo hayo hayo. 1

9Kwa pumzi ya Mungu huangamizwa; 2 kwa mshindo wa hasira zake huangamia. 1

10Simba anaweza kunguruma na kukoroma, 2 lakini bado meno ya simba mkubwa huvunjika. 1

11Simba anaweza kuangamia kwa kukosa mawindo, 2 nao wana wa simba jike hutawanyika. 1

12“Neno lililetwa kwangu kwa siri, 2 masikio yangu yakasikia mnongʼono wake. 1

13Katikati ya ndoto za kutia wasiwasi wakati wa usiku, 2 hapo usingizi mzito uwapatapo wanadamu, 1

14hofu na kutetemeka kulinishika 2 na kufanya mifupa yangu yote itetemeke. 1

15Kuna roho aliyepita mbele ya uso wangu, 2 nazo nywele za mwili wangu zikasimama. 1

16Yule roho akasimama, 2 lakini sikuweza kutambua kilikuwa kitu gani. 1 Umbo fulani lilisimama mbele ya macho yangu, 2 kukawa na ukimya kisha nikasikia sauti: 1

17‘Je, binadamu aweza kuwa mwadilifu kuliko Mungu? 2 Je, mtu aweza kuwa safi kuliko Muumba wake? 1

18Kama Mungu hawaamini watumishi wake, 2 kama yeye huwalaumu malaika zake kwa kukosea, 1

19ni mara ngapi zaidi wale waishio katika nyumba 2 za udongo wa mfinyanzi, 1 ambazo misingi yake ipo mavumbini, 2 ambao wamepondwa kama nondo! 1

20Kati ya mawio na machweo 2 huvunjwa vipande vipande; 1 bila yeyote kutambua, 2 huangamia milele. 1

21Je, kamba za hema yao hazikungʼolewa, 2 hivyo hufa bila hekima?’

← Job 3Read In The App, Free →Job 5 →

Study Job 4

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142