Job · Biblia (Kiswahili)

Job 34

1Kisha Elihu akasema: 1

2“Sikieni maneno yangu, enyi watu wenye hekima; 2 nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye maarifa. 1

3Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno 2 kama vile ulimi uonjavyo chakula. 1

4Tujichagulie wenyewe yaliyo sawa, 2 nasi tujifunze pamoja yaliyo mema. 1

5“Ayubu anasema, ‘Mimi sina hatia, 2 lakini Mungu ameninyima haki yangu. 1

6Ingawa niko sawa, 2 ninaonekana mwongo; 1 nami ingawa sina kosa, 2 kidonda changu hakiponi.’ 1

7Ni mtu gani aliye kama Ayubu, 2 anywaye dharau kama maji? 1

8Ashirikianaye na watenda mabaya 2 na kuchangamana na watu waovu. 1

9Kwa kuwa anasema, ‘Haimfaidi mwanadamu kitu chochote 2 anapojitahidi kumpendeza Mungu.’ 1

10“Hivyo nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye ufahamu. 2 Kamwe Mungu hatendi uovu, 2 Mwenyezi hafanyi kosa. 1

11Humlipa mwanadamu kwa ajili ya lile alilotenda; 2 huleta juu yake kile ambacho matendo yake yanastahili. 1

12Ni jambo lisiloweza kufikiriwa kwamba Mungu angefanya makosa, 2 kwamba Mwenyezi angepotosha hukumu. 1

13Je, ni nani aliyemtawaza juu ya dunia? 2 Ni nani aliyemweka kuwa mwangalizi wa ulimwengu wote? 1

14Kama lilikuwa kusudi la Mungu, 2 naye akaiondoa Roho yake na pumzi yake, 1

15wanadamu wote wangeliangamia kwa pamoja, 2 na mtu angerudi mavumbini. 1

16“Kama ninyi mnaufahamu, sikieni hili; 2 sikilizeni hili nisemalo. 1

17Je, yeye aichukiaye haki aweza kutawala? 2 Je, utamhukumu mwenye haki, Aliye na Nguvu Zote? 1

18Je, si ni yeye awaambiaye wafalme, ‘Ninyi hamfai kitu,’ 2 nao watu mashuhuri, ‘Ninyi ni waovu,’ 1

19yeye asiyependelea wakuu, 2 wala haonyeshi upendeleo kwa matajiri kuliko maskini, 2 kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake? 1

20Wanakufa ghafula, usiku wa manane; 2 watu wanatikiswa nao hupita; 1 wenye nguvu huondolewa 2 bila mkono wa mwanadamu. 1

21“Macho yake yanazitazama njia za wanadamu; 2 anaona kila hatua yao. 1

22Hakuna mahali penye giza nene, wala uvuli mkubwa, 2 ambapo watenda mabaya wanaweza kujificha. 1

23Mungu hana haja ya kumchunguza mtu sana, 2 ili apate kuja mbele zake kwa hukumu. 1

24Bila kuuliza huwapondaponda wenye nguvu nyingi 2 na kuwaweka wengine mahali pao. 1

25Kwa sababu huyaangalia matendo yao yote, 2 huwaondoa usiku, nao wakaangamia. 1

26Anawaadhibu kwa ajili ya uovu wao 2 mahali ambapo kila mmoja ataweza kuwaona, 1

27kwa sababu wameacha kumfuata Mungu, 2 nao hawakuiheshimu njia yake hata moja. 1

28Wamesababisha kilio cha maskini kifike mbele zake, 2 hivyo akasikia kilio cha wahitaji. 1

29Lakini kama akinyamaza kimya, 2 ni nani awezaye kumhukumu? 1 Kama akiuficha uso wake, 2 ni nani awezaye kumwona? 1 Ikiwa ni taifa au mtu mmoja, kwake ni sawa, 2

30ili kumzuia mtu mwovu kutawala, 2 au wale ambao huwategea watu mitego. 1

31“Kama mwanadamu akimwambia Mungu, 2 ‘Nimekosa lakini sitatenda dhambi tena. 1

32Nifundishe nisichoweza kuona; 2 kama nimekukosea, sitafanya hivyo tena.’ 1

33Je basi, Mungu atakulipa kwa masharti yako, 2 wakati wewe umekataa kutubu? 1 Yakupasa wewe uamue, wala si mimi; 2 sasa niambie lile ulijualo. 1

34“Wanadamu wenye ufahamu husema, 2 wenye hekima wanaonisikia huniambia, 1

35‘Ayubu huongea bila maarifa; 2 maneno yake hayana busara.’ 1

36Laiti Ayubu angejaribiwa hadi kikomo cha mwisho, 2 kwa sababu anajibu kama mtu mwovu! 1

37Kwenye dhambi yake huongeza uasi; 2 kwa dharau hupiga makofi miongoni mwetu, 2 na kuzidisha maneno yake dhidi ya Mungu.”

← Job 33Read In The App, Free →Job 35 →

Study Job 34

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142