Job · Biblia (Kiswahili)

Job 21

1Ndipo Ayubu akajibu: 1

2“Yasikilizeni maneno yangu kwa makini; 2 hii na iwe faraja mnayonipa mimi. 1

3Nivumilieni ninapozungumza, 2 nami nikishazungumza, endeleeni kunidhihaki. 1

4“Je, kwani malalamiko yangu yanaelekezwa kwa mwanadamu? 2 Kwa nini nisikose subira? 1

5Niangalieni mkastaajabu; 2 mkaweke mkono juu ya vinywa vyenu. 1

6Ninapowaza juu ya hili, ninaogopa, 2 nao mwili wangu unatetemeka. 1

7Kwa nini waovu wanaendelea kuishi, 2 wakifikia umri wa uzee na kuendelea kuwa na nguvu? 1

8Huwaona watoto wao wakithibitika 2 wakiwa wamewazunguka, 2 wazao wao mbele za macho yao. 1

9Nyumba zao zi salama wala hakuna hofu; 2 fimbo ya Mungu haiko juu yao. 1

10Madume yao ya ngʼombe huvyaza bila kushindwa kamwe; 2 ngʼombe wao huzaa wala hawaharibu mimba. 1

11Huwatoa watoto wao nje kama kundi; 2 wadogo wao huchezacheza. 1

12Huimba nyimbo kwa matari na kwa kinubi, 2 nao huifurahia sauti ya filimbi. 1

13Huitumia miaka yao katika mafanikio 2 nao hushuka kaburini kwa amani. 1

14Lakini humwambia Mungu, ‘Tuache sisi!’ 2 Hatuna haja ya kufahamu njia zako. 1

15Mwenyezi ni nani hata tumtumikie? 2 Tutapata faida gani kumwomba? 1

16Lakini kufanikiwa kwao hakupo mikononi mwao wenyewe, 2 hivyo najitenga mbali na shauri la waovu. 1

17“Lakini ni mara ngapi taa ya waovu huzimwa? 2 Ni mara ngapi maafa huwajia, 1 yale yawapatayo ambayo Mungu 2 huwapangia katika hasira yake? 1

18Ni mara ngapi huwa kama majani makavu mbele ya upepo, 2 kama makapi yachukuliwayo na dhoruba? 1

19Imesemekana, ‘Mungu huiweka akiba adhabu ya mtu 2 kwa ajili ya wanawe.’ 1 Mungu na amlipe mtu mwenyewe, 2 ili apate kulijua! 1

20Macho yake mwenyewe na yaone maangamizi yake; 2 yeye na ainywe ghadhabu ya Mwenyezi. 1

21Kwani anajali nini kuhusu jamaa anayoiacha nyuma, 2 miezi yake aliyopangiwa ifikapo mwisho? 1

22“Je, yuko mtu yeyote awezaye kumfundisha Mungu maarifa, 2 iwapo yeye ndiye ahukumuye hata walio juu ya wote? 1

23Mtu mmoja hufa akiwa na nguvu zake kamili, 2 akiwa salama na mwenye raha kamili, 1

24mwili wake ukiwa umenawiri, 2 nayo mifupa yake ikiwa imejaa mafuta ndani yake. 1

25Mtu mwingine hufa katika uchungu wa nafsi, 2 akiwa hajafurahia kamwe jambo lolote zuri. 1

26Hao wote hulala mavumbini, 2 nao mabuu huwafunika wote. 1

27“Ninayajua kikamilifu yale mnayoyafikiri, 2 mipango ambayo kwayo mngenitendea mabaya. 1

28Mwasema, ‘Iko wapi sasa nyumba ya huyo mtu mkuu, 2 mahema ambayo watu waovu walikaa?’ 1

29Je, hamkuwahi kuwauliza hao wanaosafiri? 2 Je, hamkutafakari taarifa zao: 1

30kwamba mtu mwovu huepushwa kutoka siku ya maafa, 2 kwamba huokolewa kutoka siku ya ghadhabu? 1

31Ni nani hulaumu matendo yake mbele ya uso wake? 2 Ni nani ampatilizaye kwa yale aliyoyatenda? 1

32Hupelekwa kaburini, 2 nao ulinzi ukawekwa kwenye kaburi lake. 1

33Udongo ulio bondeni ni mtamu kwake; 2 watu wote watamfuata, 2 nao umati wa watu usiohesabika umemtangulia. 1

34“Hivyo ninyi mnawezaje kunifariji kwa upuzi wenu? 2 Hakuna kilichosalia cha majibu yenu isipokuwa uongo!”

← Job 20Read In The App, Free →Job 22 →

Study Job 21

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142