Job 27
1Ndipo Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema: 1
2“Hakika kama Mungu aishivyo, aliyeninyima haki yangu, 2 Mwenyezi ambaye amenifanya 2 nionje uchungu wa nafsi, 1
3kwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu, 2 nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu, 1
4midomo yangu haitanena uovu, 2 wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu. 1
5Sitakubaliana nanyi kabisa kuwa mko sahihi; 2 hadi nife, sitakana uadilifu wangu. 1
6Nitadumisha haki yangu wala sitaiacha; 2 dhamiri yangu haitanisuta muda wote ninaoishi. 1
7“Watesi wangu wawe kama waovu, 2 nao adui zangu wawe kama wasio haki! 1
8Kwa maana mtu asiyemcha Mungu 2 analo tegemeo gani anapokatiliwa mbali, 2 Mungu anapouondoa uhai wake? 1
9Je, Mungu husikiliza kilio chake, 2 shida zimjiapo? 1
10Je, anaweza kumfurahia Mwenyezi? 2 Je, atamwita Mungu nyakati zote? 1
11“Nitawafundisha juu ya uweza wa Mungu; 2 njia za Mwenyezi sitazificha. 1
12Ninyi nyote mmeona hili wenyewe. 2 Ni ya nini basi mazungumzo haya yasiyo na maana? 1
13“Hili ndilo fungu ambalo Mungu humpa mtu mwovu, 2 urithi ule mtu mdhalimu anapokea kutoka kwa Mwenyezi: 1
14Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani, 2 fungu lao ni kuuawa kwa upanga; 1 wazao wake hawatakuwa kamwe 2 na chakula cha kuwatosha. 1
15Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao, 2 nao wajane wao hawatawaombolezea. 1
16Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, 2 na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi, 1
17yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, 2 naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake. 1
18Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui, 2 kama kibanda alichotengeneza mlinzi. 1
19Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho; 2 afunguapo macho yake, yote yametoweka. 1
20Vitisho humjia kama mafuriko; 2 dhoruba humkumba ghafula usiku. 1
21Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka; 2 humzoa kutoka mahali pake. 1
22Humvurumisha bila huruma, 2 huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake. 1
23Upepo humpigia makofi kwa dharau, 2 na kumfukuza atoke mahali pake.