Job 23
1Ndipo Ayubu akajibu: 1
2“Hata leo malalamiko yangu ni chungu; 2 mkono wake ni mzito juu yangu hata nikiugua. 1
3Laiti ningefahamu mahali pa kumwona; 2 laiti ningeweza kwenda mahali akaapo! 1
4Ningeliweka shauri langu mbele zake, 2 na kukijaza kinywa changu na hoja. 1
5Ningejua kwamba angenijibu nini, 2 na kuelewa lile ambalo angelisema. 1
6Je, angenipinga kwa nguvu nyingi? 2 La, asingenigandamiza. 1
7Hapo mtu mwadilifu angeweka shauri lake mbele zake, 2 nami ningeokolewa milele na mhukumu wangu. 1
8“Lakini nikienda mashariki, hayupo; 2 nikienda magharibi, simpati. 1
9Anapokuwa kazini pande za kaskazini, simwoni; 2 akigeukia kusini, nako simwoni hata kidogo. 1
10Lakini anaijua njia niiendeayo; 2 akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. 1
11Nyayo zangu zimefuata hatua zake kwa karibu; 2 nimeishika njia yake bila kukengeuka. 1
12Sijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake; 2 nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku. 1
13“Lakini yeye husimama peke yake; ni nani awezaye kumpinga? 2 Yeye hufanya lolote atakalo. 1
14Hutimiliza maagizo yake dhidi yangu, 2 na bado anayo mipango mingi kama hiyo ambayo ameiweka akiba. 1
15Hiyo ndiyo sababu ninaingiwa na hofu mbele zake; 2 nifikiriapo haya yote ninamwogopa. 1
16Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia; 2 yeye Mwenyezi amenitia hofu. 1
17Hata hivyo sijanyamazishwa na giza, 2 wala kwa giza nene linalofunika uso wangu.