Job · Biblia (Kiswahili)

Job 22

1Ndipo Elifazi Mtemani akajibu: 1

2“Je, mwanadamu aweza kuwa wa faida kwa Mungu? 2 Je, hata mtu mwenye hekima aweza kumfaidi? 1

3Je, Mwenyezi angefurahia nini 2 kama ungekuwa mwadilifu? 1 Au je, yeye angepata faida gani 2 kama njia zako zingekuwa kamilifu? 1

4“Je, ni kwa ajili ya utaua wako ndiyo maana anakukemea 2 na kuleta mashtaka dhidi yako? 1

5Je, uovu wako si mkuu? 2 Dhambi zako si hazina mwisho? 1

6Umedai dhamana kwa ndugu zako bila sababu; 2 umewavua watu nguo zao, ukawaacha uchi. 1

7Hukumpa maji aliyechoka, 2 nawe ulimnyima chakula mwenye njaa, 1

8ingawa ulikuwa mtu mwenye uwezo ukimiliki nchi: 2 mtu uliyeheshimiwa, ukiishi ndani yake. 1

9Umewafukuza wajane mikono mitupu 2 na kuzivunja nguvu za yatima. 1

10Ndiyo sababu mitego imekuzunguka pande zote, 2 hatari ya ghafula inakutia hofu, 1

11ndiyo sababu ni giza sana huwezi kuona, 2 tena ndiyo sababu mafuriko ya maji yamekufunika. 1

12“Je, Mungu hayuko katika mbingu za juu? 2 Juu kuliko nyota zilizo juu sana! 1

13Hivyo wewe wasema, ‘Mungu anajua nini?’ 2 Je, yeye huhukumu katika giza kama hilo? 1

14Mawingu mazito ni pazia lake, hivyo hatuoni sisi 2 atembeapo juu ya anga la dunia. 1

15Je, utaifuata njia ya zamani, 2 ambayo watu waovu waliikanyaga? 1

16Waliondolewa kabla ya wakati wao, 2 misingi yao ikachukuliwa na mafuriko. 1

17Walimwambia Mungu, ‘Tuache sisi! 2 Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?’ 1

18Lakini ndiye alizijaza nyumba zao na vitu vizuri, 2 hivyo ninajitenga mbali na mashauri ya waovu. 1

19“Wenye haki wanaona maangamizi yao na kufurahi, 2 nao wasio na hatia huwadhihaki, wakisema, 1

20‘Hakika adui zetu wameangamizwa, 2 nao moto umeteketeza mali zao.’ 1

21“Mjue sana Mungu ili uwe na amani, 2 ndipo mema yatakapokujia. 1

22Uyapokee mafundisho toka kinywani mwake, 2 na maneno yake uyaweke moyoni mwako. 1

23Kama ukimrudia Mwenyezi, utarudishwa upya: 2 Kama ukiuondoa uovu uwe mbali na hema lako, 1

24kama dhahabu yako ukiihesabu kama mavumbi, 2 dhahabu yako ya Ofiri kama miamba ya mabondeni, 1

25ndipo Mwenyezi atakuwa dhahabu yako, 2 naye atakuwa fedha yako iliyo bora. 1

26Hakika ndipo utakapojifurahisha kwa Mwenyezi, 2 nawe utamwinulia Mungu uso wako. 1

27Utamwomba yeye, naye atakusikia, 2 nawe utazitimiza nadhiri zako. 1

28Utakusudia jambo nalo litatendeka, 2 nao mwanga utaangazia njia zako. 1

29Watu watakaposhushwa, nawe ukasema, ‘Wainue!’ 2 ndipo atamwokoa aliyevunjika moyo. 1

30Atamwokoa hata yule ambaye ana hatia, 2 ataokolewa kwa sababu ya usafi wa mikono yako.”

← Job 21Read In The App, Free →Job 23 →

Study Job 22

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142