Job 17
1Moyo wangu umevunjika, 2 siku zangu zimefupishwa, 2 kaburi linaningojea. 1
2Hakika wenye mizaha wamenizunguka; 2 macho yangu yamebaki kutazama uadui wao. 1 Ayubu Anaomba Msaada 1
3“Ee Mungu, nipe dhamana unayodai. 2 Ni nani mwingine atakayeweka dhamana kwa ajili yangu? 1
4Umezifunga akili zao zisipate ufahamu, 2 kwa hiyo hutawaacha wapate ushindi. 1
5Kama mtu akiwashutumu rafiki zake ili apate ujira, 2 macho ya watoto wake yatashindwa kuona. 1
6“Mungu amenifanya kitu cha dhihaka kwa kila mtu, 2 mtu ambaye watu humtemea mate usoni. 1
7Macho yangu yamefifia kwa ajili ya majonzi; 2 umbile langu lote ni kama kivuli. 1
8Watu wanyofu wanatishwa na hili; 2 watu wasio na hatia wanasimama dhidi ya wasiomcha Mungu. 1
9Hata hivyo, waadilifu watazishika njia zao, 2 nao wale wenye mikono safi wataendelea kupata nguvu. 1
10“Lakini ninyi njooni, ninyi nyote, jaribuni tena! 2 Sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu. 1
11Siku zangu zimepita, mipango yangu imevunjika, 2 vivyo hivyo shauku za moyo wangu. 1
12Watu hawa hufanya usiku kuwa mchana, 2 kwenye giza wao husema, ‘Mwanga u karibu.’ 1
13Kama nyumba pekee ninayoitarajia ni kaburi, + 17:13 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. 2 kama nikikitandika kitanda changu gizani, 1
14kama nikiuambia uharibifu, ‘Wewe u baba yangu,’ 2 na kuliambia buu, ‘Wewe u mama yangu’ au ‘Dada yangu,’ 1
15liko wapi basi tarajio langu? 2 Ni nani awezaye kuona tarajio lolote kwa ajili yangu? 1
16Je, litashuka chini hadi kwenye malango ya mauti? + 17:16 Malango ya mauti hapa ina maana ya Kuzimu. 2 Je, tutashuka pamoja mavumbini?”