Job 41
1“Je, waweza kumvua Lewiathani + 41:1 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. kwa ndoano ya samaki, 2 au kufunga ulimi wake kwa kamba? 1
2Waweza kupitisha kamba puani mwake, 2 au kutoboa taya lake kwa kulabu? 1
3Je, ataendelea kukuomba umhurumie? 2 Atasema nawe maneno ya upole? 1
4Je, atafanya agano nawe ili umtwae 2 awe mtumishi wako maisha yake yote? 1
5Je, utamfuga na kumfanya rafiki kama ndege, 2 au kumfunga kamba kwa ajili ya wasichana wako? 1
6Je, wafanyabiashara watabadilishana bidhaa kwa ajili yake? 2 Watamgawanya miongoni mwa wafanyao biashara? 1
7Je, waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha kali, 2 au kichwa chake kwa mkuki wa kuvulia samaki? 1
8Kama ukiweka mkono wako juu yake, 2 utavikumbuka hivyo vita na kamwe hutarudia tena! 1
9Tumaini lolote la kumtiisha ni kujidanganya; 2 kule kumwona tu kunamwangusha mtu chini. 1
10Hakuna yeyote aliye mkali athubutuye kumchokoza. 2 Ni nani basi awezaye kusimama dhidi yangu? 1
11Ni nani mwenye madai dhidi yangu ili nipate kumlipa? 2 Kila kitu kilicho chini ya mbingu ni mali yangu. 1
12“Sitashindwa kunena juu ya maungo yake, 2 nguvu zake na umbo lake zuri. 1
13Ni nani awezaye kumvua gamba lake la nje? 2 Ni nani awezaye kumsogelea na lijamu? 1
14Nani athubutuye kuufungua mlango wa kinywa chake, 2 kilichozungukwa na meno yake ya kutisha pande zote? 1
15Mgongo wake una safu za ngao 2 zilizoshikamanishwa imara pamoja; 1
16kila moja iko karibu sana na mwenzake, 2 wala hakuna hewa iwezayo kupita kati yake. 1
17Zimeunganishwa imara kila moja na nyingine; 2 zimengʼangʼaniana pamoja wala haziwezi kutenganishwa. 1
18Akipiga chafya mwanga humetameta; 2 macho yake ni kama mionzi ya mapambazuko. 1
19Mienge iwakayo humiminika kutoka kinywani mwake; 2 cheche za moto huruka nje. 1
20Moshi hufuka kutoka puani mwake, 2 kama kutoka kwenye chungu kinachotokota kwa moto wa matete. 1
21Pumzi yake huwasha makaa ya mawe, 2 nayo miali ya moto huruka kutoka kinywani mwake. 1
22Nguvu hukaa katika shingo yake; 2 utisho hutangulia mbele yake. 1
23Mikunjo ya nyama yake imeshikamana imara pamoja; 2 iko imara na haiwezi kuondolewa. 1
24Kifua chake ni kigumu kama mwamba, 2 kigumu kama jiwe la chini la kusagia. 1
25Ainukapo, mashujaa wanaogopa; 2 hurudi nyuma mbele yake anapokwenda kwa kishindo. 1
26Upanga unaomfikia haumdhuru, 2 wala mkuki au mshale wala fumo. 1
27Chuma hukiona kama unyasi, 2 na shaba kama mti uliooza. 1
28Mishale haimfanyi yeye akimbie; 2 mawe ya kombeo kwake ni kama makapi. 1
29Rungu kwake huwa kama kipande cha jani kavu; 2 hucheka sauti za kugongana kwa mkuki. 1
30Sehemu zake za chini kwenye tumbo 2 zina menomeno na mapengo kama vigae vya chungu, 1 zikiacha mburuzo kwenye matope 2 kama chombo chenye meno cha kupuria. 1
31Huvisukasuka vilindi kama sufuria kubwa ichemkayo, 2 na kukoroga bahari kama chungu cha marhamu. 1
32Anapopita nyuma yake huacha mkondo unaometameta; 2 mtu angedhani vilindi vilikuwa na mvi. 1
33Hakuna chochote duniani kinacholingana naye: 2 yeye ni kiumbe kisicho na woga. 1
34Yeye huwatazama chini wale wote wenye kujivuna; 2 yeye ni mfalme juu ya wote wenye kiburi.”