Job · Biblia (Kiswahili)

Job 13

1“Macho yangu yameona hili lote, 2 masikio yangu yamesikia na kulielewa. 1

2Hayo mnayoyajua mimi pia ninayajua; 2 mimi si mtu duni kuliko ninyi. 1

3Lakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi 2 na kuhojiana shauri langu na Mungu. 1

4Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo; 2 ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote! 1

5Laiti wote mngenyamaza kimya! 2 Kwa kuwa kwenu hilo lingekuwa hekima. 1

6Sikieni sasa hoja yangu; 2 sikilizeni kusihi kwangu. 1

7Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu? 2 Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake? 1

8Mtamwonyesha upendeleo? 2 Mtamtetea Mungu kwenye mashtaka yake? 1

9Je, ingekuwa vyema Mungu akiwahoji ninyi? 2 Je, mngeweza kumdanganya kama ambavyo mngeweza kuwadanganya wanadamu? 1

10Hakika angewakemea 2 kama mkiwapendelea watu kwa siri. 1

11Je, huo ukuu wake haungewatisha ninyi? 2 Je, hofu yake isingewaangukia ninyi? 1

12Maneno yenu ni mithali za majivu; 2 utetezi wenu ni ngome za udongo wa mfinyanzi. 1

13“Nyamazeni kimya nipate kusema; 2 kisha na yanipate yatakayonipata. 1

14Kwa nini nijiweke mwenyewe kwenye hatari 2 na kuyaweka maisha yangu mikononi mwangu? 1

15Ingawa ataniua, bado nitamtumaini; 2 hakika nitazitetea njia zangu mbele zake. 1

16Naam, hili litanigeukia kuwa wokovu wangu, 2 kwa maana hakuna mtu asiyemcha Mungu 2 atakayethubutu kuja mbele yake! 1

17Sikilizeni maneno yangu kwa makini; 2 nayo masikio yenu yaingize kile nisemacho. 1

18Sasa kwamba nimekwisha kutayarisha mambo yangu, 2 ninajua mimi nitahesabiwa kuwa na haki. 1

19Je, kuna yeyote anayeweza kuleta mashtaka dhidi yangu? 2 Kama ndivyo, nitanyamaza kimya na nife. 1

20“Ee Mungu, unijalie tu mimi haya mambo mawili, 2 nami sitajificha uso wako: 1

21Ondoa mkono wako uwe mbali nami, 2 nawe uache kuniogofya kwa hofu zako kuu. 1

22Niite kwenye shauri nami nitajibu, 2 au niache niseme, nawe upate kujibu. 1

23Ni makosa na dhambi ngapi nilizotenda? 2 Nionyeshe kosa langu na dhambi yangu. 1

24Kwa nini kuuficha uso wako 2 na kunihesabu mimi kuwa adui yako? 1

25Je, utaliadhibu jani lipeperushwalo na upepo? 2 Je, utayasaka makapi makavu? 1

26Kwa kuwa unaandika mambo machungu dhidi yangu 2 na kunifanya nizirithi dhambi za ujana wangu. 1

27Umeifunga miguu yangu kwenye pingu. 2 Unazichunga kwa makini njia zangu zote 2 kwa kutia alama kwenye nyayo za miguu yangu. 1

28“Hivyo mwanadamu huangamia kama kitu kilichooza, 2 kama vazi lililoliwa na nondo.

← Job 12Read In The App, Free →Job 14 →

Study Job 13

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142