Job 38
1Kisha Bwana akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema: 1
2“Nani huyu atiaye mashauri yangu giza 2 kwa maneno yasiyo na maarifa? 1
3Jikaze kama mwanaume; 2 nitakuuliza swali, 2 nawe unijibu. 1
4“Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia? 2 Niambie, kama unafahamu. 1
5Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake? 2 Hakika wewe unajua! 2 Ni nani aliyenyoosha kamba ya kupimia juu yake? 1
6Je, misingi yake iliwekwa juu ya nini, 2 au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni, 1
7wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, 2 na malaika wote walipokuwa wakipiga kelele kwa furaha? 1
8“Ni nani aliyeifungia bahari milango 2 ilipopasuka kutoka tumbo, 1
9nilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake, 2 na kuyafungia katika giza nene, 1
10nilipoamuru mipaka yake, 2 na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake, 1
11niliposema, ‘Unaweza kufika mpaka hapa wala si zaidi; 2 hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’? 1
12“Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke, 2 au kuyaonyesha mapambazuko mahali pake, 1
13yapate kushika miisho ya dunia, 2 na kuwakungʼuta waovu waliomo? 1
14Dunia hubadilika kama udongo wa mfinyanzi chini ya lakiri; 2 sura yake hukaa kama ile ya vazi. 1
15Waovu huzuiliwa nuru yao, 2 nao mkono wao ulioinuliwa huvunjwa. 1
16“Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari? 2 Au kutembea mahali pa ndani pa vilindi? 1
17Umewahi kuonyeshwa malango ya mauti? 2 Umewahi kuiona milango ya uvuli wa mauti? 1
18Je, wewe unafahamu ukubwa wa dunia? 2 Niambie kama unajua haya yote. 1
19“Njia ya kufika kwenye makao ya nuru ni ipi? 2 Nako maskani mwa giza ni wapi? 1
20Je, unaweza kuvirudisha kwenye makao yake? 2 Unajua njia za kufika maskani mwake? 1
21Hakika unajua, kwa kuwa ulikuwa umeshazaliwa! 2 Kwani umeishi miaka mingi! 1
22“Je, umeshawahi kuingia katika ghala za theluji, 2 au kuona ghala za mvua ya mawe, 1
23ambazo nimeziweka akiba kwa ajili ya wakati wa taabu, 2 na kwa ajili ya wakati wa vita na mapigano? 1
24Ni ipi njia iendayo mahali umeme wa radi unapotawanyiwa, 2 au mahali upepo wa mashariki unaposambaziwa juu ya dunia? 1
25Ni nani aliyepasua mifereji kwa ajili ya maji mengi ya mvua yaendayo kasi 2 na njia ya umeme wa radi, 1
26ili kusababisha mvua kunyeshea mahali pasipokaliwa na mtu, 2 jangwa lisilo na yeyote ndani yake, 1
27ili kuitosheleza nchi ya ukiwa na jangwa, 2 na majani yaanze kumea ndani yake? 1
28Je, mvua ina baba? 2 Ni nani baba azaaye matone ya umande? 1
29Barafu inatoka tumbo la nani? 2 Ni nani azaaye ukungu kutoka mbinguni, 1
30wakati maji yawapo magumu kama jiwe, 2 wakati uso wa vilindi vya maji unapoganda? 1
31“Je, waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia? 2 Waweza kulegeza kamba za Orioni? 1
32Waweza kuyaongoza makundi ya nyota kwa majira yake, 2 au kuongoza Dubu na watoto wake? 1
33Je, unajua sheria zinazotawala mbingu? 2 Waweza kuweka utawala wa Mungu duniani? 1
34“Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni, 2 na kujifunika mwenyewe na gharika ya maji? 1
35Je, wewe hutuma umeme wa radi kwenye njia zake? 2 Je, hutoa taarifa kwako kukuambia, ‘Sisi tuko hapa’? 1
36Ni nani aliyeujalia moyo hekima 2 au kuzipa akili ufahamu? 1
37Nani mwenye hekima ya kuyahesabu mawingu? 2 Ni nani awezaye kuinamisha magudulia ya mbinguni 1
38wakati mavumbi yawapo magumu, 2 na mabonge ya udongo kushikamana pamoja? 1
39“Je, utamwindia simba jike mawindo, 2 na kuwashibisha simba wenye njaa 1
40wakati wao wamejikunyata mapangoni mwao, 2 au wakivizia kichakani? 1
41Ni nani ampaye kunguru chakula 2 wakati makinda yake yanamlilia Mungu, 2 yakizungukazunguka kwa ajili ya kukosa chakula?