Job · Biblia (Kiswahili)

Job 40

1Bwana akamwambia Ayubu: 1

2“Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha? 2 Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.”

3Ndipo Ayubu akamjibu Bwana: 1

4“Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe? 2 Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu. 1

5Nimesema mara moja, lakini sina jibu; 2 naam, nimesema mara mbili, 2 lakini sitasema tena.”

6Ndipo Bwana akasema na Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli: 1

7“Jikaze kama mwanaume; 2 nitakuuliza maswali, nawe yakupasa unijibu. 1

8“Je, utabatilisha hukumu yangu? 2 Utanilaumu mimi ili kujihesabia haki mwenyewe? 1

9Je, una mkono kama wa Mungu, 2 nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake? 1

10Basi jivike mwenyewe utukufu na fahari, 2 nawe uvae heshima na enzi. 1

11Fungulia ukali wa ghadhabu yako, 2 mtafute kila mwenye kiburi umshushe, 1

12mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze, 2 waponde waovu mahali wasimamapo. 1

13Wazike wote mavumbini pamoja; 2 wafunge nyuso zao kaburini. 1

14Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia 2 kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa. 1

15“Mwangalie mnyama aitwaye Behemothi, + 40:15 Huyu alikuwa mnyama wa nyakati za zamani ambaye hajulikani hasa ni gani. 2 niliyemuumba kama nilivyokuumba wewe, 2 anayekula majani kama ngʼombe. 1

16Tazama basi nguvu alizo nazo kwenye viuno vyake, 2 uwezo alio nao kwenye misuli ya tumbo lake! 1

17Mkia wake hutikisika kama mwerezi; 2 mishipa ya mapaja yake imesukwa pamoja. 1

18Mifupa yake ni bomba za shaba, 2 maungo yake ni kama fito za chuma. 1

19Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu, 2 lakini Muumba wake anaweza kumsogelea kwa upanga wake. 1

20Vilima humletea yeye mazao yake, 2 nao wanyama wote wa porini hucheza karibu naye. 1

21Hulala chini ya mimea ya yungiyungi, 2 katika maficho ya matete kwenye matope. 1

22Hiyo mimea ya yungiyungi humficha kwenye vivuli vyake; 2 miti mirefu karibu na kijito humzunguka. 1

23Wakati mto ufurikapo, yeye hapati mshtuko wa hofu; 2 yeye yu salama, hata kama Yordani ingefurika hadi kwenye kinywa chake. 1

24Je, mtu yeyote anaweza kumkamata yeye akiwa macho, 2 au kumnasa kwa mtego na kutoboa pua yake?

← Job 39Read In The App, Free →Job 41 →

Study Job 40

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142