Job · Biblia (Kiswahili)

Job 3

1Baada ya jambo hili, Ayubu akafumbua kinywa chake na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake.

2Kisha akasema: 1

3“Siku ya kuzaliwa kwangu na ipotelee mbali, 2 nao usiku ule iliposemekana, 2 ‘Mtoto wa kiume amezaliwa!’ 1

4Siku ile na iwe giza; 2 Mungu juu na asiiangalie; 2 nayo nuru isiiangazie. 1

5Giza na kivuli kikuu kiikalie tena; 2 wingu na likae juu yake; 2 weusi na uifunike nuru yake. 1

6Usiku ule na ushikwe na giza kuu; 2 usihesabiwe katika siku za mwaka, 2 wala usihesabiwe katika siku za mwezi wowote. 1

7Usiku ule na uwe tasa; 2 sauti ya furaha na isisikike ndani yake. 1

8Wale wazilaanio siku wailaani hiyo siku, 2 wale walio tayari kumwamsha Lewiathani. + 3:8 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. 1

9Nyota zake za alfajiri na ziwe giza; 2 nao ungojee mwanga bila mafanikio, 1 wala usiuone mwonzi wa kwanza 2 wa mapambazuko, 1

10kwa sababu huo usiku haukunifungia 2 mlango wa tumbo la mama yangu, 1 ili kuyaficha macho yangu 2 kutokana na taabu. 1

11“Kwa nini sikuangamia wakati wa kuzaliwa? 2 Kwa nini sikufa nilipokuwa ninatoka tumboni? 1

12Kwa nini pakawa na magoti ya kunipokea 2 na matiti ili nipate kunyonyeshwa? 1

13Kwa maana sasa ningekuwa nimepumzika kwa amani. 2 Ningekuwa nimelala na kupumzika 1

14pamoja na wafalme na washauri wa dunia, 2 waliojijengea mahali ambapo sasa ni magofu, 1

15pamoja na watawala waliokuwa na dhahabu, 2 waliozijaza nyumba zao kwa fedha. 1

16Au kwa nini sikufichwa ardhini kama mtoto aliyezaliwa mfu, 2 kama mtoto mchanga ambaye kamwe hakuuona mwanga? 1

17Huko waovu huacha kusumbua 2 na huko waliochoka hupumzika. 1

18Wafungwa nao hufurahia utulivu wao, 2 hawasikii tena sauti ya kukemea ya kiongozi wa watumwa. 1

19Wadogo na wakubwa wamo humo, 2 na mtumwa ameachiwa huru kutoka kwa bwana wake. 1

20“Mbona nuru inawaangazia wale walio taabuni, 2 na hao wenye uchungu kupewa uhai, 1

21wale wanaotamani kifo ambacho hakiji, 2 wale watafutao kufa zaidi ya kutafuta hazina iliyofichwa, 1

22ambao hujawa na furaha, 2 na hushangilia wafikapo kaburini? 1

23Kwa nini uhai hupewa mtu 2 ambaye njia yake imefichika, 2 ambaye Mungu amemzungushia boma? 1

24Kwa maana kulia kwangu kwa uchungu kwanijia badala ya chakula; 2 kusononeka kwangu kunamwagika kama maji. 1

25Lile nililokuwa naliogopa limenijia; 2 lile nililokuwa ninalihofia limenipata. 1

26Sina amani, wala utulivu; 2 sina pumziko, bali taabu tu.”

← Job 2Read In The App, Free →Job 4 →

Study Job 3

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142