Job 30
1“Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuniliko wananidhihaki, 1 watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau 2 kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo. 1
2Nguvu za mikono yao zingekuwa na faida gani kwangu, 2 kwa kuwa nguvu zao zilikuwa zimewaishia? 1
3Wakiwa wamekonda kutokana na kupungukiwa na kwa njaa, 2 walizurura usiku katika nchi kame iliyo ukiwa. 1
4Katika vichaka walikusanya mimea ya chumvi, 2 nacho chakula chao kilikuwa mizizi ya mti wa mfagio. 1
5Walifukuzwa mbali na watu wao, 2 wakipigiwa kelele kama wevi. 1
6Walilazimika kuishi katika mikondo ya vijito vilivyokauka, 2 kwenye majabali na mahandaki. 1
7Kwenye vichaka walilia kama punda, 2 na walijisongasonga pamoja kwenye vichaka. 1
8Wao ni watoto wa wapumbavu wenye asili ya ubaya, 2 waliofukuzwa watoke katika nchi. 1
9“Nao sasa wana wao wananidhihaki katika nyimbo; 2 nimekuwa kitu cha dhihaka kwao. 1
10Wananichukia sana na kujitenga nami, 2 wala hawasiti kunitemea mate usoni. 1
11Sasa kwa kuwa Mungu ameilegeza kamba ya upinde wangu na kunitesa, 2 wamekuwa huru kunitendea waonavyo. 1
12Kuume kwangu kundi linashambulia; 2 wao huitegea miguu yangu tanzi, 2 na kunizingira. 1
13Huizuia njia yangu, 2 nao hufanikiwa katika kuniletea maafa, 2 nami sina yeyote wa kunisaidia. 1
14Wananijia kama watu wapitao katika ufa mpana; 2 katikati ya magofu huja na kunishambulia. 1
15Vitisho vimenifunika; 2 heshima yangu imetoweshwa kama kwa upepo, 2 salama yangu imetoweka kama wingu. 1
16“Sasa maisha yangu yamefikia mwisho; 2 siku za mateso zimenikamata. 1
17Usiku mifupa yangu inachoma; 2 maumivu yanayonitafuna hayatulii kamwe. 1
18Kwa uwezo wake mkuu Mungu huwa kwangu kama nguo; 2 hushikamana nami kama ukosi wa vazi langu. 1
19Yeye amenitupa kwenye matope, 2 nami nimekuwa kama mavumbi na majivu. 1
20“Ee Bwana, ninakulilia wewe lakini hunijibu; 2 ninasimama, nawe unanitazama tu. 1
21Wewe unanigeukia bila huruma; 2 unanishambulia kwa nguvu za mkono wako. 1
22Unaninyakua na kunipeperusha kwa upepo; 2 umenirusha huku na huko kwenye dhoruba kali. 1
23Ninajua utanileta mpaka kifoni, 2 mahali ambapo wenye uhai wote wamewekewa. 1
24“Hakika hakuna yeyote amshambuliaye mhitaji, 2 anapoomba msaada katika shida yake. 1
25Je, sikulia kwa ajili ya wale waliokuwa katika taabu? 2 Je, nafsi yangu haikusononeka kwa ajili ya maskini? 1
26Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia; 2 nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja. 1
27Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii; 2 siku za mateso zinanikabili. 1
28Ninazunguka nikiwa nimeungua, lakini si kwa jua; 2 ninasimama katika kusanyiko nikiomba msaada. 1
29Nimekuwa ndugu wa mbweha, 2 rafiki wa mabundi. 1
30Ngozi yangu imekuwa nyeusi nayo inachunika; 2 mifupa yangu inaungua kwa homa. 1
31Kinubi changu kimegeuka kuwa maombolezo, 2 nayo filimbi yangu imekuwa sauti ya kilio.