Isaiah 12
1Katika siku ile utasema: 1 “Nitakusifu wewe, Ee Bwana. 2 Ingawa ulinikasirikia, 1 hasira yako imegeukia mbali 2 nawe umenifariji. 1
2Hakika Mungu ni wokovu wangu; 2 nitamtumaini wala sitaogopa. 1 Bwana, Bwana, ni nguvu zangu na wimbo wangu; 2 amekuwa wokovu wangu.” 1
3Kwa furaha mtachota maji 2 kutoka visima vya wokovu.
4Katika siku hiyo mtasema: 1 “Mshukuruni Bwana, mliitie jina lake; 2 julisheni miongoni mwa mataifa yale aliyoyafanya, 2 tangazeni kuwa jina lake limetukuka. 1
5Mwimbieni Bwana, kwa kuwa ametenda mambo makuu, 2 hili na lijulikane duniani kote. 1
6Pazeni sauti mwimbe kwa furaha, watu wa Sayuni, 2 kwa maana mkuu ni yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli miongoni mwenu.”
Study Isaiah 12
KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)