Isaiah 26
1Katika siku ile, wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda: 1 Tuna mji ulio na nguvu, 2 Mungu huufanya wokovu kuwa kuta zake na maboma yake. 1
2Fungua malango ili taifa lenye haki lipate kuingia, 2 taifa lile lidumishalo imani. 1
3Utamlinda katika amani kamilifu 2 yeye ambaye moyo wake ni thabiti 2 kwa sababu anakutumaini wewe. 1
4Mtumaini Bwana milele, 2 kwa kuwa Bwana, Bwana, ni Mwamba wa milele. 1
5Huwashusha wale wajikwezao, 2 huushusha chini mji wenye kiburi, 1 huushusha hadi ardhini 2 na kuutupa chini mavumbini. 1
6Miguu huukanyaga chini, 2 miguu ya hao walioonewa, 2 hatua za hao maskini. 1
7Mapito ya wenye haki yamenyooka. 2 Ewe uliye Mwenye Haki, 2 waisawazisha njia ya mtu mnyofu. 1
8Naam, Bwana, tukienenda katika sheria zako, 2 twakungojea wewe, 1 jina lako na sifa zako 2 ndizo shauku za mioyo yetu. 1
9Nafsi yangu yakutamani wakati wa usiku, 2 wakati wa asubuhi roho yangu yakuonea shauku. 1 Wakati hukumu zako zinapokuja juu ya dunia, 2 watu wa ulimwengu hujifunza haki. 1
10Ingawa neema yaonyeshwa kwa waovu, 2 hawajifunzi haki, 1 hata katika nchi ya unyofu huendelea kutenda mabaya 2 wala hawazingatii utukufu wa Bwana. 1
11Ee Bwana, mkono wako umeinuliwa juu, 2 lakini hawauoni. 1 Wao na waone wivu wako kwa ajili ya watu wako tena waaibishwe, 2 moto uliowekwa akiba kwa ajili ya adui zako na uwateketeze. 1
12Bwana, unaamuru amani kwa ajili yetu, 2 yale yote tuliyoweza kuyakamilisha ni wewe uliyetenda kwa ajili yetu. 1
13Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametutawala, 2 lakini jina lako pekee ndilo tunaloliheshimu. 1
14Wao sasa wamekufa, wala hawako tena hai, 2 roho za waliokufa hazitarudi tena. 1 Uliwaadhibu na kuwaangamiza, 2 umefuta kumbukumbu lao lote. 1
15Umeliongeza hilo taifa, Ee Bwana, 2 umeliongeza hilo taifa. 1 Umejipatia utukufu kwa ajili yako mwenyewe, 2 umepanua mipaka yote ya nchi. 1
16Bwana, walikujia katika taabu yao, 2 wewe ulipowarudi, 2 waliweza kuomba kwa kunongʼona tu. 1
17Kama mwanamke mwenye mimba aliyekaribia kuzaa 2 anavyogaagaa na kulia kwa ajili ya maumivu yake, 2 ndivyo tulivyokuwa mbele zako, Ee Bwana. 1
18Tulikuwa na mimba, tuligaagaa kwa maumivu, 2 lakini tulizaa upepo. 1 Hatukuleta wokovu duniani, 2 hatujazaa watu katika ulimwengu huu. 1
19Lakini wafu wenu wataishi, 2 nayo miili yao itafufuka. 1 Ninyi mnaokaa katika mavumbi, 2 amkeni mkapige kelele kwa furaha. 1 Umande wenu ni kama umande wa asubuhi, 2 dunia itawazaa wafu wake. 1
20Nendeni, watu wangu, ingieni vyumbani mwenu 2 na mfunge milango nyuma yenu, 1 jificheni kwa kitambo kidogo 2 mpaka ghadhabu yake ipite. 1
21Tazama, Bwana anakuja kutoka makao yake 2 ili kuwaadhibu watu wa dunia kwa ajili ya dhambi zao. 1 Dunia itadhihirisha umwagaji damu juu yake, 2 wala haitaendelea kuwaficha watu wake waliouawa.