Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 15

1Neno kuhusu Moabu: 1 Ari iliyo Moabu imeangamizwa: 2 imeharibiwa kwa usiku mmoja! 1 Kiri iliyo Moabu imeangamizwa, 2 imeharibiwa kwa usiku mmoja! 1

2Diboni anakwea hadi kwenye hekalu lake, 2 mpaka mahali pake pa juu ili walie, 2 Moabu anaombolezea Nebo na Medeba. 1 Kila kichwa kimenyolewa 2 na kila ndevu limeondolewa. 1

3Wamevaa nguo za magunia barabarani, 2 juu ya mapaa na kwenye viwanja 1 wote wanaomboleza, 2 wamelala kifudifudi kwa kulia. 1

4Heshboni na Eleale wanalia, 2 sauti zao zinasikika hadi Yahazi. 1 Kwa hiyo watu wenye silaha wa Moabu wanapiga kelele, 2 nayo mioyo yao imezimia. 1

5Moyo wangu unamlilia Moabu; 2 wakimbizi wake wanakimbilia Soari, 2 hadi Eglath-Shelishiya. 1 Wanapanda njia ya kwenda Luhithi, 2 wanakwenda huku wanalia; 1 barabarani iendayo Horonaimu 2 wanaombolezea maangamizi yao. 1

6Maji ya Nimrimu yamekauka 2 na majani yamenyauka; 1 mimea imekauka wala hakuna 2 kitu chochote kibichi kilichobaki. 1

7Kwa hiyo mali waliyoipata na kujiwekea akiba 2 wamezichukua na kuvuka Bonde la Mierebi. 1

8Mwangwi wa kilio chao umefika hadi mpakani mwa Moabu, 2 kilio chao cha huzuni kimefika hadi Eglaimu, 2 maombolezo yao hadi Beer-Elimu. 1

9Maji ya Dimoni yamejaa damu, 2 lakini bado nitaleta pigo jingine juu ya Dimoni: 1 simba juu ya wakimbizi wa Moabu 2 na juu ya wale wanaobaki katika nchi.

← Isaiah 14Read In The App, Free →Isaiah 16 →

Study Isaiah 15

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566