Isaiah 13
1Neno kuhusu Babeli ambalo Isaya mwana wa Amozi aliliona: 1
2Twekeni bendera juu ya mlima usio na kitu, 2 wapazieni sauti, 1 wapungieni mkono waingie 2 katika malango ya wenye heshima. 1
3Nimewaamuru watakatifu wangu; 2 nimewaita mashujaa wangu waitimize hasira yangu: 2 wale wanaoshangilia ushindi wangu. 1
4Sikilizeni kelele juu ya milima, 2 kama ile ya umati mkubwa wa watu! 1 Sikilizeni, makelele katikati ya falme, 2 kama mataifa yanayokusanyika pamoja! 1 Bwana Mwenye Nguvu Zote anakusanya 2 jeshi kwa ajili ya vita. 1
5Wanakuja kutoka nchi za mbali sana, 2 kutoka miisho ya mbingu, 1 Bwana na silaha za ghadhabu yake, 2 kuangamiza nchi yote. 1
6Ombolezeni, kwa maana siku ya Bwana i karibu, 2 itakuja kama uharibifu kutoka kwa Mwenyezi. + 13:6 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. 1
7Kwa sababu ya hili, mikono yote italegea, 2 moyo wa kila mtu utayeyuka. 1
8Hofu itawakamata, 2 uchungu na maumivu makali yatawashika, 1 watagaagaa kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa. 1 Watatazamana kwa hofu kila mtu na mwenzake, 2 nyuso zao zikiwaka kama moto. 1
9Tazameni, siku ya Bwana inakuja, 2 siku katili, yenye ghadhabu na hasira kali, 1 kuifanya nchi kuwa ukiwa 2 na kuwaangamiza wenye dhambi waliomo ndani yake. 1
10Nyota za mbinguni na makundi ya nyota 2 havitatoa mwanga wake. 1 Jua linalochomoza litatiwa giza 2 na mwezi hautatoa nuru yake. 1
11Nitauadhibu ulimwengu kwa ajili ya uovu wake, 2 waovu kwa ajili ya dhambi zao. 1 Nitakomesha majivuno ya wenye kiburi, 2 na nitakishusha kiburi cha watu wakatili. 1
12Nitawafanya wanadamu kuwa adimu kuliko dhahabu safi, 2 watakuwa wachache sana kuliko dhahabu ya Ofiri. 1
13Kwa hiyo nitazifanya mbingu zitetemeke, 2 nayo dunia itatikisika kutoka mahali pake 1 katika ghadhabu ya Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 katika siku ya hasira yake iwakayo. 1
14Kama swala awindwaye, 2 kama kondoo wasio na mchungaji, 1 kila mmoja atarudi kwa watu wake mwenyewe, 2 kila mmoja atakimbilia nchi yake ya kuzaliwa. 1
15Yeyote atakayetekwa atapasuliwa tumbo, 2 wote watakaokamatwa watauawa kwa upanga. 1
16Watoto wao wachanga watavunjwa vipande vipande 2 mbele ya macho yao; 1 nyumba zao zitatekwa 2 na wake zao watatendwa jeuri. 1
17Tazama, nitawachochea Wamedi dhidi yao, 2 ambao hawajali fedha 2 wala hawafurahii dhahabu. 1
18Mishale yao itawaangusha vijana, 2 hawatakuwa na huruma kwa watoto wachanga 2 wala hawataangalia watoto kwa huruma. 1
19Babeli, johari ya falme, 2 utukufu wa kiburi cha Wababeli, + 13:19 Wababeli hapa maana yake ni Wakaldayo. 1 itaangushwa na Mungu 2 kama Sodoma na Gomora. 1
20Hautakaliwa na watu kamwe 2 wala watu hawataishi humo kwa vizazi vyote. 1 Hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake huko, 2 hakuna mchungaji atakayepumzisha makundi yake huko. 1
21Lakini viumbe wa jangwani watalala huko, 2 mbweha watajaza nyumba zake, 1 bundi wataishi humo 2 nao mbuzi-mwitu watarukaruka humo. 1
22Fisi watalia ndani ya ngome zake, 2 mbweha ndani ya majumba yake ya kifahari. 1 Wakati wake umewadia, 2 na siku zake hazitaongezwa.