Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 44

1“Lakini sasa sikiliza, ee Yakobo, mtumishi wangu, 2 Israeli, niliyemchagua. 1

2Hili ndilo asemalo Bwana, 2 yeye aliyekuhuluku, aliyekuumba tumboni, 2 yeye atakayekusaidia: 1 Usiogope, ee Yakobo, mtumishi wangu, 2 Yeshuruni, + 44:2 Yeshuruni hapa maana yake ni Yeye aliye mnyofu, yaani Israeli (ona pia Kum 32:15 ). niliyekuchagua. 1

3Kwa maana nitamimina maji juu ya nchi yenye kiu, 2 na vijito vya maji juu ya ardhi iliyokauka; 1 nitamimina Roho wangu juu ya watoto wako, 2 nayo baraka yangu juu ya wazao wako. 1

4Nao watachipua kama manyasi katika shamba la majani, 2 kama mierezi kando ya vijito vya maji yatiririkayo. 1

5Mmoja atasema, ‘Mimi ni wa Bwana’; 2 mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; 1 vilevile mwingine ataandika juu ya mkono wake, ‘Wa Bwana,’ 2 na kujiita kwa jina la Israeli. 1 Ni Bwana, Siyo Sanamu 1

6“Hili ndilo asemalo Bwana, 2 Mfalme wa Israeli na Mkombozi, 2 Bwana Mwenye Nguvu Zote: 1 Mimi ni wa kwanza na Mimi ni wa mwisho; 2 zaidi yangu hakuna Mungu. 1

7Ni nani basi aliye kama mimi? Yeye na atangaze. 2 Yeye atangaze na kuweka mbele yangu 1 ni kitu gani kilichotokea tangu nilipoumba watu wangu wa kale, 2 tena ni nini kitakachotokea: 2 naam, yeye na atoe unabii ni nini kitakachokuja. 1

8Msitetemeke, msiogope. 2 Je, sikutangaza hili, na kutoa unabii tangu zamani? 1 Ninyi ni mashahidi wangu. 2 Je, yuko Mungu zaidi yangu mimi? 1 Hasha, hakuna Mwamba mwingine; 2 mimi simjui mwingine.” 1

9Wote wachongao sanamu ni ubatili, 2 navyo vitu wanavyovithamini havifai kitu. 1 Wale ambao wanazitetea ni vipofu, 2 ni wajinga, nao waaibika. 1

10Ni nani atengenezaye mungu na kusubu sanamu, 2 ambayo haiwezi kumfaidia kitu chochote? 1

11Yeye pamoja na wenziwe wa aina yake wataaibishwa, 2 mafundi wao si kitu ila ni wanadamu tu. 1 Wote wakusanyike pamoja na kuwa na msimamo wao, 2 watashushwa chini kwa hofu na kwa fedheha. 1

12Muhunzi huchukua kifaa 2 na kukifanyia kazi kwenye makaa ya moto, 1 hutengeneza sanamu kwa nyundo, 2 huifanyiza kwa nguvu za mkono wake. 1 Huona njaa na kupoteza nguvu zake, 2 asipokunywa maji huzimia. 1

13Seremala hupima kwa kutumia kamba 2 na huuchora mstari kwa kalamu; 1 huchonga kwa patasi 2 na kutia alama kwa bikari. 1 Huifanyiza katika umbo la binadamu, 2 la mwanadamu katika utukufu wake wote, 2 ili iweze kukaa katika sehemu yake ya ibada ya miungu. 1

14Hukata miti ya mierezi, 2 huchukua mtiriza au mwaloni. 1 Huuacha ukue miongoni mwa miti ya msituni, 2 au hupanda msunobari, nayo mvua huufanya ukue. 1

15Ni kuni ya binadamu: 2 yeye huchukua baadhi yake na kuota moto, 2 huwasha moto na kuoka mkate. 1 Lakini pia huutumia kumtengeneza mungu na akamwabudu, 2 huitengeneza sanamu na kuisujudia. 1

16Sehemu ya kuni huziweka motoni, 2 akapikia chakula chake, 2 hubanika nyama na kula hadi ashibe. 1 Huota moto na kusema, 2 “Aha! Ninahisi joto, ninaona moto.” 1

17Mabaki yake hutengeneza mungu, sanamu yake; 2 yeye huisujudia na kuiabudu. 1 Huiomba na kusema, 2 “Niokoe; wewe ni mungu wangu.” 1

18Hawajui chochote, hawaelewi chochote, 2 macho yao yamefungwa hata hawawezi kuona, 2 akili zao zimefungwa hata hawawezi kufahamu. 1

19Hakuna anayefikiri, 2 hakuna mwenye maarifa wala ufahamu wa kusema, 1 “Sehemu yake nilitumia kwa kuni; 2 hata pia nilioka mkate juu ya makaa yake, 2 nikabanika nyama na kuila. 1 Je, nifanye machukizo kwa kile kilichobaki? 2 Je, nisujudie gogo la mti?” 1

20Hujilisha kwa majivu, moyo uliodanganyika humpotosha; 2 hawezi kujiokoa mwenyewe, au kusema, 2 “Je, kitu hiki kilichoko katika mkono wangu wa kuume si ni uongo?” 1

21“Ee Yakobo, kumbuka mambo haya, 2 ee Israeli, kwa kuwa wewe ni mtumishi wangu. 1 Nimekuumba wewe, wewe ni mtumishi wangu. 2 Ee Israeli, sitakusahau. 1

22Nimeyafuta makosa yako kama wingu, 2 dhambi zako kama ukungu wa asubuhi. 1 Nirudie mimi, 2 kwa kuwa nimekukomboa wewe.” 1

23Enyi mbingu, imbeni kwa furaha, 2 kwa maana Bwana amefanya jambo hili. 2 Ee vilindi vya dunia, piga kelele. 1 Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo, 2 enyi misitu na miti yenu yote, 1 kwa maana Bwana amemkomboa Yakobo, 2 ameuonyesha utukufu wake katika Israeli. 1 Yerusalemu Kukaliwa 1

24“Hili ndilo asemalo Bwana, 2 Mkombozi wako, aliyekuumba tumboni: 1 “Mimi ni Bwana, 1 niliyeumba vitu vyote, 1 niliyezitanda mbingu peke yangu, 1 niliyeitandaza nchi mwenyewe, 1

25“mimi huzipinga ishara za manabii wa uongo, 2 na kuwatia upumbavu waaguzi, 1 niyapinduaye maarifa ya wenye hekima, 2 na kuyafanya kuwa upuzi, 1

26niyathibitishaye maneno ya watumishi wake, 2 na kutimiza utabiri wa wajumbe wake, 1 “niambiaye Yerusalemu, ‘Itakaliwa na watu,’ 2 niambiaye miji ya Yuda kuwa, ‘Itajengwa,’ 2 na kuhusu magofu yake, ‘Mimi nitayatengeneza,’ 1

27niambiaye kilindi cha maji, ‘Kauka, 2 nami nitakausha vijito vyako,’ 1

28nisemaye kuhusu Koreshi, ‘Yeye ni mchungaji wangu, 2 naye atatimiza yote yanipendezayo; 2 atauambia Yerusalemu, “Ukajengwe tena,” 2 na kuhusu Hekalu, “Misingi yake na iwekwe.” ’

← Isaiah 43Read In The App, Free →Isaiah 45 →

Study Isaiah 44

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566