Isaiah · Biblia (Kiswahili)

Isaiah 2

1Hili ndilo aliloliona Isaya mwana wa Amozi kuhusu Yuda na Yerusalemu:

2Katika siku za mwisho 1 mlima wa Hekalu la Bwana utaimarishwa 2 kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote, 1 utainuliwa juu ya vilima, 2 na mataifa yote yatamiminika huko.

3Mataifa mengi yatakuja na kusema, 1 “Njooni, twendeni mlimani mwa Bwana, 2 kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. 1 Atatufundisha njia zake, 2 ili tuweze kuenenda katika mapito yake.” 1 Sheria itatoka Sayuni, 2 neno la Bwana litatoka Yerusalemu. 1

4Atahukumu kati ya mataifa 2 na ataamua migogoro ya mataifa mengi. 1 Watafua panga zao ziwe majembe, 2 na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. 1 Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, 2 wala hawatajifunza vita tena. 1

5Njooni, enyi nyumba ya Yakobo, 2 tutembeeni katika nuru ya Bwana. 1 Siku Ya Bwana 1

6Umewatelekeza watu wako, 2 nyumba ya Yakobo. 1 Wamejaa ushirikina utokao Mashariki, 2 wanapiga ramli kama Wafilisti 2 na wanashikana mikono na wapagani. 1

7Nchi yao imejaa fedha na dhahabu, 2 hakuna mwisho wa hazina zao. 1 Nchi yao imejaa farasi, 2 hakuna mwisho wa magari yao. 1

8Nchi yao imejaa sanamu, 2 wanasujudia kazi za mikono yao, 2 vitu vile vidole vyao vimevitengeneza. 1

9Kwa hiyo mwanadamu atashushwa 2 na binadamu atanyenyekezwa: 2 usiwasamehe. 1

10Ingieni kwenye miamba, 2 jificheni ardhini 1 kutokana na utisho wa Bwana 2 na utukufu wa enzi yake! 1

11Macho ya mtu mwenye majivuno yatanyenyekezwa 2 na kiburi cha wanadamu kitashushwa, 1 Bwana peke yake ndiye atakayetukuzwa siku hiyo. 1

12Bwana Mwenye Nguvu Zote anayo siku aliyoiweka akiba 2 kwa wote wenye kujivuna na wenye kiburi, 2 kwa wote wanaojikweza 2 (nao watanyenyekezwa), 1

13kwa mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu sana, 2 na mialoni yote ya Bashani, 1

14kwa milima yote mirefu 2 na vilima vyote vilivyoinuka, 1

15kwa kila mnara ulio mrefu sana 2 na kila ukuta wenye ngome, 1

16kwa kila meli ya biashara, + 2:16 Au: ya Tarshishi (ona pia 1Fal 10:22; 22:48; 2Nya 9:21; 20:36; Isa 60:9 .) 2 na kila chombo cha baharini cha fahari. 1

17Majivuno ya mwanadamu yatashushwa, 2 na kiburi cha wanadamu kitanyenyekezwa, 1 Bwana peke yake ndiye atatukuzwa siku hiyo, 2

18nazo sanamu zitatoweka kabisa. 1

19Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba, 2 na kwenye mahandaki ardhini 1 kutokana na utisho wa Bwana 2 na utukufu wa enzi yake, 2 ainukapo kuitikisa dunia. 1

20Siku ile, watu watawatupia 2 panya na popo 1 sanamu zao za fedha na za dhahabu, 2 walizozitengeneza ili waziabudu. 1

21Watakimbilia kwenye mapango miambani 2 na kwenye nyufa za miamba 1 kutokana na utisho wa Bwana 2 na utukufu wa enzi yake, 2 ainukapo kuitikisa dunia. 1

22Acheni kumtumainia mwanadamu, 2 ambaye hana kitu ila pumzi katika pua zake. 1 Yeye ana thamani gani?

← Isaiah 1Read In The App, Free →Isaiah 3 →

Study Isaiah 2

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566