Isaiah 57
1Mwenye haki hupotea, 2 wala hakuna hata mmoja awazaye hilo moyoni mwake; 1 watu wanaomcha Mungu huondolewa, 2 wala hakuna hata mmoja anayeelewa 1 kuwa wenye haki wameondolewa 2 ili wasipatikane na maovu. 1
2Wale waendao kwa unyofu 2 huwa na amani; 2 hupata pumziko walalapo mautini. 1
3“Lakini ninyi: 2 Njooni hapa, ninyi wana wa wachawi, 2 ninyi wazao wa wazinzi na makahaba! 1
4Mnamdhihaki nani? 2 Ni nani mnayemcheka kwa dharau, 2 na kumtolea ndimi zenu? 2 Je, ninyi si watoto wa waasi, 2 uzao wa waongo? 1
5Mnawaka tamaa katikati ya mialoni 2 na chini ya kila mti uliotanda matawi; 1 mnawatoa kafara watoto wenu kwenye mabonde 2 na chini ya majabali yenye mianya. 1
6“Sanamu zilizo katikati ya mawe laini ya mabondeni ndizo fungu lenu; 2 hizo ndizo sehemu yenu. 1 Naam, kwa hizo mmemimina sadaka za vinywaji, 2 na kutoa sadaka za nafaka. 1 Katika haya yote, 2 niendelee kuona huruma? 1
7Umeweka kitanda chako juu kwenye kilima kirefu kilichoinuka, 2 huko ulikwenda kutoa dhabihu zako. 1
8Nyuma ya milango yako na miimo yako 2 umeweka alama zako za kipagani. 1 Kwa kuniacha mimi, ulifunua kitanda chako, 2 umepanda juu yake na kukipanua sana; 1 ulifanya patano na wale ambao unapenda vitanda vyao, 2 nawe uliangalia uchi wao. 1
9Ulikwenda kwa Moleki + 57:9 Moleki alikuwa mungu aliyekuwa anaabudiwa na Waamoni; pia alijulikana kama Malkomu, Maloki au Kemoshi wa Moabu. ukiwa na mafuta ya zeituni, 2 na ukaongeza manukato yako. 1 Ukawatuma wajumbe wako mbali sana, 2 ukashuka kwenye kaburi + 57:9 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. lenyewe! 1
10Ulikuwa umechoshwa na njia zako zote, 2 lakini hukusema, ‘Hakuna tumaini.’ 1 Ulipata uhuisho wa nguvu zako, 2 kwa sababu hiyo hukuzimia. 1
11“Ni nani uliyemhofu hivyo na kumwogopa 2 hata ukawa mwongo kwangu, 1 wala hukunikumbuka 2 au kutafakari hili moyoni mwako? 1 Si ni kwa sababu nimekuwa kimya muda mrefu 2 hata huniogopi? 1
12Nitaifunua haki yako na matendo yako, 2 nayo hayatakufaidi. 1
13Utakapolia kwa kuhitaji msaada, 2 sanamu zako ulizojikusanyia na zikuokoe! 1 Upepo utazipeperusha zote, 2 pumzi peke yake itazipeperusha, 1 Lakini mtu atakayenifanya kimbilio lake, 2 atairithi nchi 2 na kuumiliki mlima wangu mtakatifu.” 1 Faraja Kwa Wenye Majuto
14Tena itasemwa: 1 “Jengeni, jengeni, itengenezeni njia! 2 Ondoeni vikwazo katika njia ya watu wangu.” 1
15Kwa maana hili ndilo asemalo Aliye juu, yeye aliyeinuliwa sana, 2 yeye aishiye milele, ambaye jina lake ni Mtakatifu: 1 “Ninaishi mimi mahali palipoinuka na patakatifu, 1 lakini pia pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu 2 na mwenye roho ya unyenyekevu, 1 ili kuzihuisha roho za wanyenyekevu 2 na kuihuisha mioyo yao waliotubu. 1
16Sitaendelea kulaumu milele, 2 wala sitakasirika siku zote, 1 kwa kuwa roho ya mwanadamu 2 ingezimia mbele zangu: 2 yaani pumzi ya mwanadamu niliyemuumba. 1
17Nilighadhibika na tamaa yake ya dhambi; 2 nilimwadhibu, nikauficha uso wangu kwa hasira, 2 na bado aliendelea katika njia zake za tamaa. 1
18Nimeziona njia zake, lakini nitamponya, 2 nitamwongoza na kumrudishia upya faraja, 1
19nikiumba sifa midomoni ya waombolezaji 2 katika Israeli. 1 Amani, amani, kwa wale walio mbali 2 na kwa wale walio karibu,” 2 asema Bwana. “Nami nitawaponya.” 1
20Bali waovu ni kama bahari ichafukayo, 2 ambayo haiwezi kutulia, 2 mawimbi yake hutupa takataka na matope. 1
21Mungu wangu asema, 2 “Hakuna amani kwa waovu.”