Isaiah 50
1Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Iko wapi hati ya talaka ya mama yako 2 ambayo kwayo niliachana naye? 1 Au nimewauza ninyi kwa nani 2 miongoni mwa watu wanaonidai? 1 Kwa ajili ya dhambi zenu mliuzwa, 2 kwa sababu ya makosa, mama yenu aliachwa. 1
2Nilipokuja, kwa nini hakuwepo hata mmoja? 2 Nilipoita, kwa nini hakuwepo hata mmoja wa kujibu? 1 Je, mkono wangu ni mfupi mno hata nisiweze kuwakomboa? 2 Je, mimi sina nguvu za kukuokoa? 1 Kwa kukemea tu naikausha bahari, 2 naigeuza mito ya maji kuwa jangwa; 1 samaki wake wanaoza kwa kukosa maji 2 na kufa kwa ajili ya kiu. 1
3Ninalivika anga weusi na kufanya nguo ya gunia 2 kuwa kifuniko chake.” 1
4Bwana Mwenyezi amenipa ulimi uliofundishwa, 2 ili kujua neno limtegemezalo aliyechoka. 1 Huniamsha asubuhi kwa asubuhi, 2 huamsha sikio langu lisikie kama mtu afundishwaye. 1
5Bwana Mwenyezi amezibua masikio yangu, 2 nami sikuwa mwasi, 2 wala sikurudi nyuma. 1
6Niliwapa mgongo wangu wale wanipigao, 2 mashavu yangu wale wangʼoao ndevu zangu; 1 sikuuficha uso wangu kutokana na fedheha 2 na kutemewa mate. 1
7Kwa sababu Bwana Mwenyezi ananisaidia, 2 sitatahayarika. 1 Kwa hiyo nimekaza uso wangu kama jiwe la gumegume, 2 nami ninajua sitaaibika. 1
8Yeye anipatiaye haki yangu yu karibu. 1 Ni nani basi atakayeleta mashtaka dhidi yangu? 2 Tukabiliane uso kwa uso! 1 Mshtaki wangu ni nani? 2 Ni nani aliye mshtaki wangu? 1
9Ni Bwana Mwenyezi anisaidiaye mimi. 2 Ni nani huyo atakayenihukumu? 1 Wote watachakaa kama vazi, 2 nondo watawala wawamalize. 1
10Ni nani miongoni mwenu amchaye Bwana, 2 na kulitii neno la mtumishi wake? 1 Yeye atembeaye gizani, 2 yeye asiye na nuru, 1 na alitumainie jina la Bwana, 2 na amtegemee Mungu wake. 1
11Lakini sasa, ninyi nyote mnaowasha mioto, 2 na kupeana mienge iwakayo ninyi kwa ninyi, 1 nendeni, tembeeni katika nuru ya moto wenu 2 na ya mienge mliyoiwasha. 1 Hili ndilo mtakalolipokea kutoka mkononi mwangu: 2 Mtalala chini kwa mateso makali.