Isaiah 28
1Ole kwa lile taji la maua, kiburi cha walevi wa Efraimu, 2 kwa ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake, 1 uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba: 2 kwa ule mji, kiburi cha wale walioshushwa na mvinyo! 1
2Tazama, Bwana anaye mmoja aliye na uwezo na nguvu. 2 Kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo uharibuo, 1 kama mvua inyeshayo kwa nguvu na mafuriko yashukayo, 2 atakiangusha chini kwa nguvu. 1
3Lile taji la maua, kiburi cha walevi cha Efraimu, 2 kitakanyagwa chini ya nyayo. 1
4Lile ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake, 2 uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba, 1 litakuwa kama tini iliyoiva kabla ya mavuno: 2 mara mtu aionapo, huichuma na kuila. 1
5Katika siku ile, Bwana Mwenye Nguvu Zote 2 atakuwa taji la utukufu, 1 taji zuri la maua 2 kwa mabaki ya watu wake. 1
6Atakuwa roho ya haki 2 kwa yeye aketiye katika kiti cha hukumu, 1 chanzo cha nguvu 2 kwa wale wazuiao vita langoni. 1
7Hawa pia wanapepesuka kwa sababu ya mvinyo, 2 wanayumbayumba kwa sababu ya kileo: 1 Makuhani na manabii wanapepesuka kwa sababu ya kileo, 2 wanachanganyikiwa kwa sababu ya mvinyo; 1 wanapepesuka wanapoona maono, 2 wanajikwaa wanapotoa maamuzi. 1
8Meza zote zimejawa na matapishi 2 wala hakuna sehemu hata ndogo 2 isiyokuwa na uchafu. 1
9“Yeye anajaribu kumfundisha nani? 2 Yeye anamwelezea nani ujumbe wake? 1 Je, ni kwa watoto walioachishwa kunyonya? 2 Je, ni wale ambao ndipo tu wametolewa matitini? 1
10Kwa maana ni: 2 Amri juu ya amri, amri juu ya amri, 2 kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; 2 hapa kidogo, kule kidogo.” 1
11Sawa kabisa, kwa midomo migeni 2 na kwa lugha ngeni, 2 Mungu atasema na watu hawa, 1
12wale ambao aliwaambia, 2 “Hapa ni mahali pa kupumzika, 2 waliochoka na wapumzike,” 1 na, “Hapa ni mahali pa mapumziko,” 2 lakini hawakutaka kusikiliza. 1
13Hivyo basi, neno la Bwana kwao litakuwa: 2 Amri juu ya amri, amri juu ya amri, 2 kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni, 2 hapa kidogo, kule kidogo: 1 ili waende na kuanguka chali, 2 wakijeruhiwa, wakinaswa na kukamatwa. 1
14Kwa hiyo sikieni neno la Bwana, enyi watu wenye dharau 2 mnaotawala watu hawa wa Yerusalemu. 1
15Ninyi mnajisifu, “Tumefanya agano na mauti, 2 tumefanya mapatano na kuzimu. 1 Wakati pigo lifurikalo litakapopita, 2 haliwezi kutugusa sisi, 1 kwa kuwa tumefanya uongo kuwa kimbilio letu 2 na miungu ya uongo kuwa mahali petu pa kujificha.”
16Kwa hiyo hivi ndivyo Bwana Mwenyezi asemavyo: 1 “Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni, 2 jiwe lililojaribiwa, 1 jiwe la pembeni la thamani kwa ajili ya msingi thabiti. 2 Yeye atumainiye kamwe hatatiwa hofu. 1
17Nitaifanya haki kuwa kamba ya kupimia 2 na uadilifu kuwa timazi; 1 mvua ya mawe itafagia kimbilio lenu, huo uongo, 2 nayo maji yatafurikia mahali penu pa kujificha. 1
18Agano lenu na kifo litabatilishwa, 2 patano lenu na kuzimu halitasimama. 1 Wakati pigo lifurikalo litakapowakumba, 2 litawaangusha chini. 1
19Kila mara lijapo litawachukua, 2 asubuhi baada ya asubuhi, 1 wakati wa mchana na wakati wa usiku, 2 litawakumba tangu mwanzo hadi mwisho.” 1 Kuuelewa ujumbe huu 2 utaleta hofu tupu. 1
20Kitanda ni kifupi mno kujinyoosha juu yake, 2 nguo ya kujifunikia ni nyembamba mno 2 mtu hawezi kujifunikia. 1
21Bwana atainuka kama alivyofanya kwenye Mlima Perasimu, 2 ataghadhibika kama alivyofanya katika Bonde la Gibeoni: 1 ili kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu, 2 ili kutimiza kazi yake, kazi yake ngeni. 1
22Sasa acheni dharau zenu, 2 la sivyo minyororo yenu itakuwa mizito zaidi. 1 Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, ameniambia 2 habari za maangamizi yaliyoamriwa dhidi ya nchi yote. 1
23Sikilizeni msikie sauti yangu, 2 tegeni masikio na msikie niyasemayo. 1
24Wakati mkulima alimapo ili apande, 2 je, hulima siku zote? 1 Je, huendelea kubomoa ardhi 2 na kusawazisha udongo? 1
25Akiisha kusawazisha shamba, 2 je, hatapanyi mbegu za bizari na kutawanya jira? 1 Je, hapandi ngano katika sehemu yake, 2 shayiri katika eneo lake, 2 na nafaka nyingine katika shamba lake? 1
26Mungu wake humwelekeza 2 na kumfundisha njia iliyo sahihi. 1
27Iliki haipurwi kwa nyundo, 2 wala gurudumu la gari halivingirishwi juu ya jira; 1 iliki hupurwa kwa fimbo, 2 na jira kwa ufito. 1
28Nafaka lazima isagwe ili kutengeneza mkate, 2 kwa hiyo mtu haendelei kuipura daima. 1 Ingawa huendesha magurudumu ya gari lake la kupuria juu yake, 2 farasi wake hawasagi. 1
29Haya yote pia hutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 mwenye mashauri ya ajabu, na anayepita wote kwa hekima.