Isaiah 34
1Njooni karibu, enyi mataifa, nanyi msikilize; 2 sikilizeni kwa makini, 2 enyi kabila za watu! 1 Dunia na isikie, navyo vyote vilivyo ndani yake, 2 ulimwengu na vyote vitokavyo ndani yake! 1
2Bwana ameyakasirikia mataifa yote; 2 ghadhabu yake ni juu ya majeshi yao yote. 1 Atawaangamiza kabisa, 2 atawatia mikononi mwa wachinjaji. 1
3Waliouawa watatupwa nje, 2 maiti zao zitatoa uvundo, 2 milima itatota kwa damu zao. 1
4Nyota zote za mbinguni zitayeyuka 2 na anga litasokotwa kama kitabu, 1 jeshi lote la angani litaanguka 2 kama majani yaliyonyauka kutoka kwenye mzabibu, 2 kama tini iliyonyauka kutoka kwenye mtini. 1
5Upanga wangu umekunywa na kushiba huko mbinguni, 2 tazama, unashuka katika hukumu juu ya Edomu, 1 wale watu ambao nimeshawahukumu, 2 kuwaangamiza kabisa. 1
6Upanga wa Bwana umeoga katika damu, 2 umefunikwa na mafuta ya nyama: 1 damu ya kondoo na mbuzi, 2 mafuta kutoka figo za kondoo dume. 1 Kwa maana Bwana ana dhabihu huko Bosra, 2 na machinjo makuu huko Edomu. 1
7Nyati wataanguka pamoja nao, 2 ndama waume na mafahali wakubwa. 1 Nchi yao italowana kwa damu, 2 nayo mavumbi yataloa mafuta ya nyama. 1
8Kwa sababu Bwana anayo siku ya kulipiza kisasi, 2 mwaka wa malipo, 2 siku ya kushindania shauri la Sayuni. 1
9Vijito vya Edomu vitageuka kuwa lami, 2 mavumbi yake yatakuwa kiberiti kiunguzacho, 2 nchi yake itakuwa lami iwakayo! 1
10Haitazimishwa usiku wala mchana, 2 moshi wake utapaa juu milele. 1 Kutoka kizazi hadi kizazi itakuwa ukiwa, 2 hakuna mtu yeyote atakayepita huko tena. 1
11Bundi wa jangwani na bundi mwenye sauti nyembamba wataimiliki, 2 bundi wakubwa na kunguru wataweka viota humo. 1 Mungu atanyoosha juu ya Edomu 2 kamba ya kupimia ya machafuko matupu, 2 na timazi ya ukiwa. 1
12Watu wake wa kuheshimiwa hawatakuwa na chochote 2 kitakachoitwa ufalme huko, 2 nao wakuu wao wote watatoweka. 1
13Miiba itaenea katika ngome za ndani, 2 viwawi na michongoma itaota 2 kwenye ngome zake. 1 Itakuwa maskani ya mbweha, 2 makao ya bundi. 1
14Viumbe vya jangwani vitakutana na fisi, 2 nao mbuzi-mwitu watalia wakiitana; 1 huko viumbe vya usiku vitastarehe pia 2 na kujitafutia mahali pa kupumzika. 1
15Bundi wataweka viota huko na kutaga mayai, 2 atayaangua na kutunza makinda yake 2 chini ya uvuli wa mabawa yake; 1 pia huko vipanga watakusanyika, 2 kila mmoja na mwenzi wake.
16Angalieni katika gombo la Bwana na msome: 1 Hakuna hata mmoja katika hawa atakayekosekana, 2 hakuna hata mmoja atakayemkosa mwenzi wake. 1 Kwa kuwa ni kinywa chake Mungu kimeagiza, 2 na Roho wake atawakusanya pamoja. 1
17Huwagawia sehemu zao, 2 mkono wake huwagawanyia kwa kipimo. 1 Wataimiliki hata milele 2 na kuishi humo kutoka kizazi hadi kizazi.